Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara amesema kwamba mchezaji wa timu ya Yanga Ibrahimu Ajib ni mzuri lakini hapendi kufanya mazoezi na pia kubaki katika kiwango bora kwa muda mrefu.
Manara amezungumza hayo April 18, katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za kijamii ya EATV na kuongeza kwamba licha ya kipaji alichonacho lakini anashindwa kukilinda kwa kufanya juhudi mazoezini
“Ibrahim Ajib anaanza vizuri msimu halafu ikifika mahali akishakua Mfalme katika timu anapumzika, halafu Ajib hapendi mazoezi, hawezi kucheza mechi saba mfululizo katika kiwango cha juu kwasababu hapendi mazoezi , kama angependa mazoezi ni mzuri mara tatu zaidi ya Mbwana Samatta”, alisema Manara
Kwa upande mwingine Manara amesisitiza kwamba Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye nidhamu ukilinganisha na wachezaji wengine waliotoka timu ya Simba na kuhamia kwa wapinzani wao Yanga.
No comments:
Post a Comment