Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amezindua zoezi la utoaji wa
chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) ikihusisha Wasichana wenye
umri wa Miaka 14.
RC
Makonda amesema zoezi hilo litaanza rasmi Jumatatu ya February 23 likihususisha
zaidi ya Wasichana 24,097 ambao watakaopata chanjo hiyo katika vituo 270
ikiwemo shule na mitaa.
Aidha
RC Makonda amesema utoaji wa chanjo hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana
na ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukisababisha vifo vya kinamama wengi
huku akiitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara.
Pamoja
na hayo RC Makonda ametoa wito kwa viongozi wa dini, madiwani, wenyeviti wa
mitaa na wajumbe kuhamasisha jamii kwenda kupata chanjo hiyo.
Hata
hivyo RC Makonda amesema chanzo cha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni
pamoja na mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuzaa watoto wengi
pamoja na uvutaji wa sigara ambapo dalili zake ni kutokwa na damu bila
mpangilio, maumivu ya mgongo, miguu, kiuno, kutokwa na uchafu ukeni pamoja na
kuchoka, kupungua uzito na hamu ya kula.
RC
Makonda amesema Saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa na virusi vya Human
Papilloma ambapo kinga yake kwa hatua ya mwanzo ni kufanyiwa uchunguzi wa kina
ili kubaini dalili za mwanzo na kupata matibabu stahiki.
Chanjo
ya Saratani ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2018 itatolewa kwa
wasichana wanaotimiza umri wa miaka 14 ambao wamezaliwa kuanzia January 01 hadi
Disemba 31 mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment