Mtu mmoja Mkazi wa Mnazimmoja
barabara ya Sukuma na Mafya jijini Dar es Salaam
anayefahamika kwa jina la Wechu Salumu Abdallah amemlili Mkuu wa Mkoa huo Mhe.
Paul Makonda amsaidie kwani amedhulumiwa nyumba na kupigwa mnada .
Akizungumza na waandishi wa habari
Bi. UWechu Abdallah amesema anamwomba mkuu wa mkoa asikie kilio chake kwani
amedhulumiwa nyumba ambayo ni ya urithi,waliyoaachiwa ambapo wapo ndugu wanne
wanayomiliki nyumba hiyo.
Amesema nyumba hiyo ya Urithi
amezelumiwa na MTU anayefahamika kwa jina la Mushi Mtakwa mwenye kampuni
inayotambulika MOSAM COMPANY ambaye alikubaliana naye kujenga ghoropha 8 ambazo
wangegawana lakini baadae wamegeuka na kuchukua nyumba hiyo na kuipiga mnada
ambapo ametakiwa kuweka zuio kwa siku 14 tu.
"Mkuu wa mkoa naomba unisaidie
Mimi mnyonge nimeachiwa watoto nawahudumia hakuna anayenisaidia hivyo nakuomba
mkuu wa mkoa wangu unisaidie nipate haki"
Ameeleza kuwa yeye pamoja na ndugu
zake hao walioachiwa nyumba hiyo walikubali kuwa mjenzi huyo ajenge ghorofa izo
8 ambapo wangegawana 4 kwa 4 na kufuatia makubaliano hayo walifuata misingi
yote ya sheria na wakaandikishana kwa makubaliano ya kujenga ghorofa.
Amendelea kusema mmoja wa mrithi wa
Mali hizo aliamua kuondoka kwenye mkataba na kutaka apewe gawio la fedha zake
ambazo ni takribani ya shilingi Milioni 70 na laki 6 ambapo walimweleza mjenzi
wao na kukubali kumpatika kasi hicho cha fedha wakaandikishiana na wakampatia
kiasi cha fedha hizo lakini Dada yao Huyo alitaka kuongezewa.
Amesema
wamwambia kuwa anataka kuongezewa hivyo wakaenda mahakamani na kuhakikisha
wakafanya makubaliano ambapo mjenzi huyo aliwapatia fedha hizo na kumpatia Dada
yao,na baada ya hapo walitakiwa kumwondoa katika makubaliano.
Aidha
mama huyu amemwomba RC Makonda kumsaidia kwani nyumba hiyo tayari imeuzwa na
mnada ulifanyika bila ya matangazo yoyote na wakati kesi bado uko mahakamani.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Baragashi Azimio amesema ni kweli nyumba hiyo
imepigwa mnada na watu waliofika kuleta tangazo ofisini kwake na kupigwa mnada
pasipokuwa na matangazo kwa wananchi wa mtaa huo kuwa nyumba inauzwa .
Nyumba
hiyo iliyopo Mtaa wa Sukuma Kariakoo Ilala jijini Dar es Salaam ilipigwa mnada
na kuuzwa kwa thamani ya shilingi milioni 350 ambapo walifanya mnada bila ya
kumshirikishwa Msimamizi wa Mirathi hiyo.
Hii ndio nyuma inayodaiwa kuzurumiwa mama huyo
No comments:
Post a Comment