A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 20, 2018

Rais Mstaafu Kikwete, Ridhiwani washindwa kuhudhuria Harusi ya Ali Kiba


Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete washindwa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Hayo yameleezwa na mtoto wa Rais Kikwete na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa mjini Dodoma anapohudhuria vikao vya Bunge.

Ridhiwan amesema kuwa, walipewa mwaliko wa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Ali kiba, lakini Rais mstaafu Kikwete kwa sasa anahudhuria shughuli nyingine Marekani, naye Ridhiwani anahudhuria vikao na shughuli mbalimbali bungeni mjini Dodoma hivyo wameshindwa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki huyo Kenya.

 Awali Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Asma Said alisema kuwa baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi, ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages