Hitmaker wa ngoma ‘Kivuruge’, Nandy a.k.a African Princess amesema moja ya vitu asivyovipenda katika muziki wake ni kuingia katika beef na msanii mwingine.
Muimbaji huyu ameiambia Clouds TV kuwa yeye sio msanii wa kupenda ugomvi na yeyote anayetaka ugomvi kwake huwa anampuuzia.
“Mimi sio mtu wa ugomvi wa mara kwa mara kwa hiyo sitamani kuingia kwenye ugomvi na mtu. Huwa napuuzia kwa kumuonyesha kuwa anachokifanya ni cha kijinga sifuatili, yaani Simuonyeshi kuwa nimeshtushwa na kitu ambacho anakifanya au labda nakifuatilia,” amesema Nandy.
Utakumbuku kumekuwa na stori zinazodai kuwa Nandy na Ruby wana beef, hata hivyo wote wawili wamekuwa wakikanusha hilo kila wanapoulizwa na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment