Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki ambao ulikuwa umekwama tumboni mwa mwanamume mmoja kwa siku sita.
David Charo alikuwa akipiga mswaki alipoumeza kimakosa Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi.
Kufikia jana, alikuwa ameanza kupata matatizo ya kupumua., Awali, madaktari walikuwa wamedokeza kwamba angehitaji kufanyiwa upasuaji kuutoa.
Lakini Ijumaa asubuhi, madaktari wakiondozwa na Ramadhan Omar wamefanikiwa kuutoa mswaki huo bila kumfanyia upasuaji wa kawaida, Badala yake, wamemfanyia upasuaji wa kutumia matundu madogo.
Jumapili, Charo alipokuwa alipoumeza mswaki huo kimakosa, awali ulikwama ndani ya koo kabla ya kutumbukia ndani tumboni.
Juhudi za nduguye mdogo Julius Charo za kuutoa hazikufanikiwa na ikalazimu wamkimbize hospitali iliyokuwa karibu.
"Tulipompeleka kwenye hospitali hiyo, madaktari walitushauri kumleta katika hospitali hii ya Pwani ambapo alipigwa picha ya x-ray, lakini kwa muda hakufanyiwa matibabu yoyote," Bw Julius aliambia gazeti la Nation.
Sima ambayo Charo alikuwa ameila usiku wa kuamkia Jumapili kilikuwa ndicho chakula chake cha mwisho mango kwake kufanikiwa kula, Amekuwa akitegemea vinywaji pekee.
"Ninaweza tu kulala au kusimama. Siwezi kujikunja au kuinama. Ninapojaribu kujipinda, nausikia mswaki ukinibana," alisema awali alipokuwa anahojiwa na gazeti la Nation.
Akizungumza na gazeti la kibinafsi la Star awali, Bw Charo alikuwa amesema amekuwa akiutumia mswaki huo kupiga mswaki kwa miaka 20.
"Ni makosa tu kwamba uliteleza kutoka mikononi mwangu Jumapili. Lakini hali yangu ni nzuri," alisema.
No comments:
Post a Comment