MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita atakuwa miongoni mwa watazamaji wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga.
Mchezo huo wa Amina yake utachezwa leo saa 10 jioni katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Meya wa jiji Mwita atakuwa miongoni mwa watazamaji wa mtanange huo mkali ambao huo kuwa na watazamaji wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na Wabunge
Ifahamike kuwa Mwita ni miongoni mwa maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu .
Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.
Imetolewa leo Aprili 29 na Christina Mwagala , Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji
No comments:
Post a Comment