AKIANZA kukinoa kwa mara ya kwanza, Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Mcongo Zahera Mwinyi amekiangalia kikosi hicho mazoezini kwa saa mbili na kutamka kuwa amevutiwa na viwango vya wachezaji aliowakuta huku akisema shughuli imeisha.
Kocha huyo alitua nchini alfajiri ya Jumapili iliyopita akitokea Kongo kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo akirithi mikoba ya Mzambia, George Lwandamina aliyesitisha mkataba wake wa kuendelea kukinoa kikosi hicho kabla ya kujiunga na Zesco ya Zambia.
Mkongoman huyo mwenye uraia wa Ufaransa mara baada ya kutua nchini aliomba kwenda kuiona timu hiyo kambini Morogoro ilipokuwepo timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa watani wa jadi, Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera alisema ameshangazwa na viwango hivyo vya wachezaji alivyovikuta huku akivutiwa na fitinesi, pumzi ambavyo ndiyo vitu muhimu kwenye timu katika kupata ushindi.
Amesema baada ya kuona viwango vya wachezaji katika kuelekea mechi dhidi ya Simba amepanga kuwaongezea vitu viwili ili kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri katika mchezo huo wa watani wa jadi ambavyo ni mbinu za kulinda na kushambulia na mfumo wake.
“Kama unakumbuka mara ya mwisho tulivyoongea hotelini kabla ya kuja kambini Morogoro, niliomba niende nikaitazame kwanza timu baada ya hapo mengine yafuate ya mimi kusaini mkataba wa kuifundisha
“Hicho ndicho nilichokifanya, nashukuru nimefika kambini salama na haraka nikaanza kuifundisha timu kwa saa mbili kwa ajili ya kuangalia kikosi, lakini imekuwa ‘sapraizi’ kwangu kukuta wachezaji wengi vijana wenye uwezo mkubwa.
“Kwa siku hizi tatu nitakazokaa na timu kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi zitatosha kwangu kuwaongezea baadhi ya vitu vichache nilivyoviona ambavyo wachezaji wangu wanahitaji kuongezewa, sitaki nikivuruge kikosi,” alisema Zahera.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, April 28, 2018
Kocha mpya Yanga avutiwa na viwango vya wachezaji
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment