A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 3, 2018

KWA MARA YA KWANZA FA AMFAGILIA JIDE

MARA baada ya kushuka jukwaani katika shoo ya Anaweza iliyofanyika usiku wa kuamkia Aprili Mosi, ndani ya Ukumbi wa Police Officers Mess uliopo Oysterbay jijini Dar, kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka mitano, mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘FA’ alimfagilia mkongwe mwenzake, Judith Wambura ‘JayDee’ kuwa ameonesha ukakamavu kuandaa shoo kivyake bila kutegemea promota.

Kwa muda mrefu, FA na JayDee walikuwa ‘hawapikiki chungu kimoja’ huku chanzo kikitajwa ni kuharibiana kwenye kuandaa shoo, lakini kipindi cha hivi karibuni wawili hao walipatana baada ya kupostiana mitandaoni kazi zao, shoo ya Anaweza imewaleta tena karibu zaidi.

Katika usiku huo, JayDee ndiye aliyemkaribisha jukwaani FA na kuimba naye baadhi ya ngoma walizotamba nazo ambapo walikumbushia Ngoma ya Msiache Kuongea na Hawajui huku shangwe zikiwa za kutosha jukwaani ‘mixer’ mapichapicha ya kamera za simu mpanguso.

Akichonga na Star Showbiz, mara baada ya kushuka jukwaani, FA alianza kwa kumfagilia JayDee; “Wasanii wakubwa kiwango cha Lady JayDee walitakiwa kuwa na shoo zao siyo kutegemea mapromota wawaandalie, kwa hiyo kitu kilichonivutia kwake na kuamua kumsapoti ni kitendo cha kuandaa shoo mwenyewe,” alisema FA.

Kivutio kikubwa kwenye shoo hiyo kilikuwa kwa mkongwe mwingine wa Bongo Fleva, Bushoke ambaye aliwa-kumbusha mashabiki kwa kibao chake cha zamani cha Usiende Mbali Nami. JayDee alipiga nyimbo zake nyingi kama vile Ndi Ndi Ndi, Sawa na Wao na mwisho alimaliza kwa kuutambulisha wimbo wake wa Anaweza alioshirikiana na mkongwe wa Muziki wa Reggae kutoka Jamaika, Luciano.

Sapraiz nyingine katika usiku huo wa Anaweza alikuwa Ben Pol ambaye aliingia na kuimba ‘live band’ vibao vyake kadhaa kama vile Maneno, Phone na Moyo Mashine.Msanii Alawi Junior pamoja na Nikki Mbishi nao walipamba usiku huo kwa kuliteka jukwaa.
STAR SHOWBIZ.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages