A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 19, 2018

CBA yatoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 10 kwa wateja wake

Mkurugengi Mkuu wa Benki ya biasahara ya CBA hapa nchini Dk Gift Shoko, akizungumza na wateja wa mkoa wa mwanza kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana na kubadilishana mawazo iliofanyika jijini Mwanza.




Mkurugengi Mkuu wa Benki ya biasahara ya CBA hapa nchini Dk Gift Shoko, akisalimiana  na wateja wa mkoa wa mwanza kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana nakubadilishana mawazo iliofanyika jijini Mwanza.
Wateja wa  Benki ya biasahara ya CBA mkoani Mwanza wakifuatilia hotuba mbalimbali jijini Mwanza,kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana na kubadilishana mawazo.
Mkurugenzi wa wateja binafsi na Masoko wa  Benki ya biasahara ya CBA  Julius Konyani, akizungumza na wateja wa mkoa wa mwanza kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana na kubadilishana mawazo iliofanyika jijini Mwanza. 
Wafanyakazi wa Benki ya biasahara ya CBA  na baadhi ya wateja wao wa mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja,kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana na kubadilishana mawazo.

Huduma ya M-Pawa inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo yenye thamani ya Sh10 bilioni kwa wateja wake katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.

Huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na kampuni ya simu ya Vodacom, imepata muitikio kutokana na Watanzania kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote walipo kwa kutumia simu za mkononi.

Zaidi ya wateja millioni 7 nchini wamejiunga na huduma hiyo ya M-Pawa na kuwawezesha wananchi wengi kupata mikopo inayowasaidia kupambana na umaskini

Akizungumza katika hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo jijini Mwanza juzi, Mkurugenzi wa benki hiyo, Gift Shoko alisema benki hiyo itaendelea kuwekeza kwenye teknolojia ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa wateja pamoja na kuongeza kasi na ufanisi.

“Wananchi lazima waendane na mabadiliko ya teknolojia ili kujikwamua kiuchumi kama vile matumizi ya simu na mitandao ili kurajisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi na mitandao,” alisema  

Aliongeza kuwa kupitia huduma ya M-Pawa wananchi wengi hawatumii muda mwingi katika kufuatilia mikopo kwenye benki.

Akizungumzia ufungwaji wa matawi manne katika jiji la Dar es Salaam eneo la Kariakoo, Mkurugenzi huyo alisema matawi hayo ya benki yalikuwa yamekaribiana huku wakilenga kujikita katika kutoa huduma kwa njia ya mtandao.

Mmoja wa wateja waliohudhuria hafla hiyo, Julius Stephen aliiomba benki hiyo kufungua matawi mengi mkoani Mwanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Naye meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Adam Makaka alisema wanalenga kuongeza kiwango cha utolewaji wa mikopo kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kutokana na kuwepo kwa biashara nyingi ndogondogo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages