Zaidi ya vikundi vya wajasiriamali 100 kunufaika na huduma ya Timiza Vikoba na Mafunzo ya Tehama
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeviasa vikundi vya kina mama wajasiriamali kutumia fursa wanazozitoa kupitia bidhaa na huduma mbalimbali za kibunifu ikiwemo Timiza Vikoba ili kujiendesha kidigital na kukuza biashara zao.
Hayo yalisemwa na meneja miradi wa Airtel Bi Jane Matinde wakati wa mkutano wa viongozi wa vikundi vya kina mama wajasiriamali jijini Dar uliondaliwa na Star Women group.
Akitoa ufafanuzi wa kina Matinde alisema “Timiza vikoba ni huduma inayowawezesha vikundi kuweka na kuchukua mikopo kupitia simu zao za mkononi kwa kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayotolewa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Maendeleo.
Timiza Vikoba inaviwezesha vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50 kujisaji na kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu”.
Matinde aliwashauri wanawake hao wajarisiamali kutumia njia za teknologia ya kisasa katika kufanya miamala ya kifedha kwa usalama, uhakika na urahisi zaidi kupitia huduma ya Timiza Vikoba “ huduma hii itawarahisishia sana kutuma pesa za michango na marejesho kupitia simu, itaokoa muda wa kukutana na kuweka uwazi kwani kila mwana kikundi anapoweka pesa fedha au kuomba mkopo kila moja anapata taarifa hapohapo nakuridhia, nawahimiza mchangamkie fursa hii.
Pamoja na huduma ya Timiza pia tunawawezesha kupata mafunzo ya Tehama kupitia maabara ya kompyuta ya Airtel fursa iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama. Tayari tunao wajasiriamali ambao wanaendelea kunufaika na masomo haya hivvo hii pia ni fursa kwenu kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi. Mafunzo haya ya Tehama yatawawezesha kutunza rekodi na mahesabu ya biashara vizuri zaidi, kutumia aplikesheni mbalimbali kuendesha biashara zenu kwa ufanusi na kukuza mitaji alisisitiza Matinde
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Star Women group na mwandaji wa mkutano huo, Bi Queen Cuthbert Sendiga aliwashukuru sana Airtel kwa kuwapatia wakinamama hao wajasiriamali fursa kupitia huduma na bidhaa zao na kuwaomba waendelea kushirikiana nao katika kutoa fursa hizi zitakazowainua wakina mama kwani ndio muhimili wa familia na kichochoe kikubwa katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla. Aidha aliahidi kuwahamasisha kina mama wengi kujiunga na masomo ya Tehama kwani uelewa bado ni Mdogo na pia kutumia technologia ya kisasa katika kuweka na kukopa kupitia huduma ya Timiza Vikoba.
Tangu kuzinduliwa kwa huduma ya Timiza Vikoba wachama zaidi ya 261,673 na vikundi 26,158 vimeshajiandikisha huku mikopo zaidi ya 774 yenye thamani ya shilingi milioni 49 kutolewa kwa vikundi hivyo
No comments:
Post a Comment