Mkurugenzi Mkuu wa TMJ Hospital, Dk. Tayabal Jafferji, akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho wa Siku Figo Duniani. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wagonjwa wa Figo, Syed Chambala.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TMJ Hospital, Bi. Parul Chhaya, akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wagonjwa wa Figo, Syed Chambala, katika ni Mkurugenzi Mkuu wa TMJ Hospital, Dk. Tayabal Jafferji,
Daktari Msaafu Martini, Sebalua ambae ni mgonjwa wa figo akiongea wakati wa halfa ya kuwafariji wagonjwa wa figo, iliyoandaliwa na Hospital ya TMJ—kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani.
Wagonjwa wa figo nchini wameiomba
serikali ya awamu ya tano kuongeza juhudi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa
figo kwa kupeleka huduma na vifaa katika hospitali za mikoani na wilayani.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya figo
duniani iliyoandaliwa na hospitali ya TMJ, Mwenyekiti wa wagonjwa wa figo
wanaotibiwa katika hospitali hiyo, Ndugu Syed Chambala alisema ni muhimu kwa
serikali kuweka mkazo wa kupambana na
ugonjwa huo.
“Ugonjwa wa figo bado haujawekea
mkazo wa kutosha na serikali yetu kwa sababu huduma na vifaa vya kusafishia
figo bado vinapatikana mjini Dar es Salaam pekee na inawalazimu wagonjwa kutoka
mikoani kuingia gharama kubwa ili kuweza kupata matibabu hayo,” aliongeza
Ndugu Chambala alisisitiza kwamba
lazima kuwe na kipaumbele katika kupambana na ugonjwa wa figo nchini na ni
muhimu kukawa na utaratibu wa kupatikana na fedha ili wagonjwa wa mikoani waweze
kusafirishwa.
Alisistiza kwamba ni muhimu
serikali ikapanua wigo wa huduma na matibabu ya figo ili kupunguza mzigo kwa
wagonjwa wanaopaswa kusafiri kuja jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
“Kwa kweli huduma za hospitali
hii ya TMJ ni za kuridhisha sana kwa wagonjwa wa figo na kitengo chao cha
huduma hii kipo imara ( Dialysis Unit) na upatikanaji wa dawa hospitali hapo ni
wa asilimia 90,” alieleza kwa wanahabari waliohudhuria shughuli hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt Tayabali Jafferji alisema kwamba hospitali hiyo
imeungana na jumuiya za kimataifa katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa
huo ambao unakua kwa kasi duniani.
Aliongeza kwamba hospitali yao
inapokea kutoka sehemu mbalimbali nchini na wameweza kuboresha vyumba na vifaa
vya kuhudumia wagonjwa ili kuwapa matumaini mapya ya kuishi maisha ya furaha.
“leo hospitali yetu inaadhimisha
siku ya figo duniani na tumewaleta wagonjwa na ndugu zao kuja kufurahi kwa
pamoja na kuwapa faraha mpya katika maisha kwamba wanaweza kuendelea kuwa na
maisha ya furaha,” alisisitiza Dkt Jafferji
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji
Mkuu wa hospitali hiyo, Bi Parul Chhaya alifafanua kwamba ugonjwa wa figo
unahitaji nguvu ya pamoja kati ya hospitali binafsi na serikali katika
kupambana nao.
“Kwa sasa tuna wagonjwa 72 wa
figo kwenye hospitali yetu na tunaendelea kupokea wengine na kwetu sisi huduma
kwanza na si pesa mbele katika harakati za kuokoa maisha ya watanzania
wenzetu,” alisema Bi Chhaya.
Naye Meja Mstaafu wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambaye ni mgonjwa wa figo, Sauka Nguluo Kullaya
aliongeza kwamba ni muhimu kwa serikali kuongeza vituo maalum kwenye hospitali
za mikoani na wilayani ili wagonjwa wa pembezoni waanze kupata huduma hizo.
Picha matukio mbalimbali katika hafla hiyo
No comments:
Post a Comment