A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 7, 2018

Tani 28 za vitunguu swaumu zateketezwa

KITENGO cha Ukaguzi cha Wizara ya Kilimo, Maliasili Mifugo na Uvuvi, kimeteketeza tani 28 za vitunguu swaumu vilivyoharibika.

Kaimu wa kitengo cha mazao ya kilimo cha Bandari ya Malindi, Mjini Unguja, Hawa Ahmada Iddi, alisema vitunguu hivyo viliingizwa nchini mwaka jana kutoka China na kuharibika baada ya kukosa hewa.

Vitunguu hivyo vilikuwa vimehifadhiwa katika makontena mawili na viliteketezwa Unguja Ukuu, Mkoa wa Kusini Unguja.

''Tumekamata makontena mawili yakiwa na vitunguu swaumu vikiwa tayari vimeharibika na tumeviteketeza,'' alisema.

Aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanaingiza bidhaa za matumizi ya kula zikiwa nzima ili kuepuka usumbufu na hasara.

Alisema serikali imeweka sheria kali ya udhibiti wa bidhaa ikiwa na lengo la kumlinda mlaji na kuepuka matumizi ya chakula vilivyopita muda wake.

''Serikali imepitisha sheria kali ya kumlinda mlaji na kudhibiti bidhaa za vyakula ziliopo katika hatari ya kuharibika na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao,'' alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages