Mahakama Kuu ya Tanzania imemuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),
kuwasilisha majibu yake kuhusu kesi za Kikatiba zilizofunguliwa na
wananchi 28 ikiwemo kupinga Jeshi la Polisi kuzuia maandamano.
Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili wa wananchi hao Jebrah
Kambole amesema mashauri hayo ya Kikatiba ni namba 4 na 6 ya 2018 ambapo
yamepangwa kusikilizwa April 5,2018.
Kambole amesema mahakama hiyo ilipanga kuanza kusikiliza mashauri hayo
leo March 9, lakini imeshindikana kwa sababu baadhi ya majaji
wamepangiwa kesi nyingine.
Kambole amesema kuwa mahakama imemuamuru AG kuwasilisha majibu yake kuhusu mashauri hayo March 21,2018.
“Mashauri haya ya yanapinga sheria mbalimbali ikiwemo kupinga sheria ya
uchaguzi, pia Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamia wa Uchaguzi
wakati inapaswa kuwepo tume huru ya Uchaguzi,”.
Wakili Kambole amesema kwenye shauri namba 4 wananchi hao 28 wanapinga
sheria za Jeshi la Jeshi la Polisi na vyama vya siasa ambazo zinatoa
muongozo wa kuzuia mikutano ya Kisiasa na kusababisha madhara mengi kwa
wananchi.
“Hivyo kimsingi tunapinga sheria hizo ambazo ni kandamizi na zinakiuka
misingi ya Katiba, ibara ya 18 Uhuru wa kujieleza kufanya mamuzi juu ya
maisha ya Watanzania na nchi,”.
Pia sheria hizo zinakiuka haki ya kusikilizwa kwa watu wanaotoa taarifa
kwa Jeshi la Polisi wakitaka kuandamana wanapata amri kabla ya
kusikilizwa, hivyo kimsingi tunaangalia uhalali wa hizo sheria kwa
Katiba yetu ya Tanzania.
“Kwa mujibu wa Ibara ya 16 inatoa majibu kwa mtu yoyote anayeona sheria imekiukwa ana wajibu wa kuleta shauri Mahakamani.
Mahakama imeyapanga mashauri hayo kuanza kutajwa April 5, 2018.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, March 9, 2018
Mwanasheria Mkuu Kupandishwa Mahakamani Kujibu Shauri la Maandamano
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment