Baada ya siku ya uvumi wa siku nyingi, imethibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.
Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na China na Korea Kaskazini, ndiyo ya
kwanza inayofahamika ya Bw Kim nje ya taifa lake tangu alipochukua
mamlaka mwaka 2011.
Bw Kim alifanya "mazungumzo ya kufana" na kiongozi wa China Xi Jinping
mjini Beijing, shirika la habari la China, Xinhua liliripoti.
China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya
wachambuzi wanasema uwezekano wa wawili hao kabla ya mkutano mkuu wa Bw
Kim na viongozi wa Korea Kusini na Marekani ulitarajiwa.
Bw Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.
Ziara hiyo ya Beijing inatazamwa na wengi kama hatua muhimu katika maandalizi ya Korea Kaskazini kuhusu mazungumzo hayo.
Wakati wa ziara hiyo, Bw Kim alimhakikishia mwenzake wa China kwamba
amejitolea kuacha kustawisha silaha za nyuklia, kwa mujibu wa shirika la
habari la Xinhua.
Hata hivyo, alisema atafanya hivyo bila masharti.
"Suala la kumalizwa kwa silaha za nyuklia katika Rais ya Korea linaweza
kutatuliwa, lakini iwapo tu Korea Kusini na Marekani watajibu juhudi
zetu kwa nia njema, kuunda mazingira ya amani na uthabiti na pia kwa
kuchukua hatua za kusonga mbele kwa pamoja kutoka kwa wadau wote
kuhakikisha amani inapatikana," Bw Kim alinukuliwa akisema.
Uhusiano na Beijing
Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, lilieleza ziara hiyo kama
yenye umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na
China.
"Ina maana kwa Korea Kaskazini kufafanua msimamo wake na kushirikiana na
China, mshirika wake muhimu zaidi," msomu katika Pacific Forum CSIS
Andray Abrahamian ameambia BBC.
"Uhusiano huo umekuwa ukidhoofika katika miaka mitano iliyopita na China
imekuwa imetengwa kidiplomasia katika miezi kadha iliyopita," amesema.
"Kutoka kwa mtazamo wa Beijing, hii ni ziara ambayo ilifaa kufanyika kitambo sana."
Kwa sehemu kubwa, hii ni ziara yenye maana kubwa kwa urafiki wa Korea
Kaskazini na China, na ni ishara ya heshima pia, Fyodor Tertitskiy wa
shirika la habari la NK News linaloangazia sana taarifa kuhusu Korea
Kaskazini alisema.
"Wana mikutano miwili mikubwa kati ya kiongozi wao na mataifa mengine -
mmoja na Seoul na mwingine na Washington - na pengine wanataka kuusikia
msimamo wa China pia.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, March 28, 2018
China na Korea Kaskazini zathibitisha Kim Jong-un ndiye aliyezuru China
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment