A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, February 4, 2018

Yanga yapata pigo la kumkosa golikipa


Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga wamepata pigo la kumkosa golikipa wao namba moja Youthe Rostand kutokana na kuwa majeruhi.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa Rostand ambaye ni raia wa Cameroon hatakuwa sehemu ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara Jumanne wiki ijayo dhidi ya timu ya Njombe Mji.

Youthe Rostand aliumia goti kwenye mchezo wa jana ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC ya Iringa na kupatiwa huduma ya matibabu ya awali kabla ya leo kupandishwa ndege kurejea Dar es salaam kwaajili ya matibabu zaidi.

Kipa huyo ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea African Lyon ya Dar es salaam amedaka mechi zote za yanga msimu huu lakini jana baada ya kuumia alimpisha mlinda mlango chipukizi Ramadhani Kabwili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages