A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 14, 2018

WAZIRI KUU RC MAKONDA WALETA FARAJA KWA MAMA NA MTOTO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa jengo la mama na mtoto lililojengwa katika hospital ya Amana  (wa pili kutoka kushot ni Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, wengine ni viongozi mbalimbali waserikali pamoja na uongozi wa kampuni ya Amsons Group. uzinduzi huo umefanyika leo jijin Dar es Salaam.

Hili ndilo jengo la mama na mtoto lililozinduliwa leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Waziri Mkuu Kassi Majaliwa wakiwa wamewabeba watoto mapacha waliozaliwa katika hospital ya Amana jijini hapa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alipowasili katika hospital ya  Amana kwaajili ya uzinduzi wa jengo la mama na mtoto uzinduzi huo umefanyika leo.

.............................


SERIKALI imesema itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini   kwa kujenga  vituo vya afya na zahanati, hospitali za rufaa pamoja na upatikanaji wa dawa lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma nzuri.

Hayo yamesemwa leo na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa akizindua Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana iliyopo Halimashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salama ambapo Wodi hiyo imejengwa kwa udhamini wa kampuni ya Amsons Group Limited,  kwa  thamani ya sh.bilioni 1.2.

Waziri  Mkuu amesema  dhamira ya serikali ni kuona wananchi  wanapata huduma za afya kwa urahisi na  kwa ukaribu mahali popote nchini na kusema kuwa serikali imedhamiria kujenga zahanati katika kila kijiji nchini, kujenga kituo cha afya katika kila kata ambapo kitakuwa kama kituo cha rufaa cha zahanati zote ndani ya kata.

“Tutahakikisha hospitali zote za  mikoa zinaingizwa kuwa chini ya Wizara ya Afya ili ziratibiwe moja kwa moja na wizara,”amesema Majaliwa.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuzipandisha hadhi hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala  ili ziwe za rufaa  ili kusaidia upatikanaji wa huduma kwa ukaribu zaidi.

Amesema  miundo mbinu ya Afya itaendelea kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya kisasa  katika hospitali za Mloganzila,  jijini Dar es Salaam, Benjamin Mkapa , Dodoma  na hospitali zote za kanda.

“Sula la afya ni moja ya mpango kipaumbele vya serikali. Tuko katika utekelezaji wa ujenzi wa  vituo vya afya, ambapo kutoka  6321  mwaka 2010 hadi  vituo 7680 mwaka 2016 likiwa ni ongezeko la asilimia  6.9,”alisema Majaliwa.

Amesema Rais  John Magufuli ametenga sh.bilioni  131 kuboresha vituo vya afya katika kata kwa kujenga wodi ya kinamama na chumba cha upasuaji  kwa  wajawazito wanaojifungua na kuongeza kuwa vituo hivyo vitakuwa na sehemu ya  magonjwa ya kawaida , maabara na nyumba ya mtumishi.

 Waziri Mkuu amesema Rais Dk. John Magufuli  ametoa sh.bilioni  bilioni 129 kwaajili ya kununua vifaa vya  tiba ambapo kila kituo kitapata mgao wa sh.milini  280.

Pia amesema serikali ilitoa magari ya wagonjwa 70 na kuyagawa  vijijini  ambapo wanatarajia kuleta magari mengine  120, na imekusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa  kwa kuwa na bejeti inayo kidhi mahitaji.

“Tunatambua changamoto ya upungufu wa watumishi hasa baada ya kuondoa wafanyakazi hewa. Serikali itaendelea kuajiri wafanyakazi  zaidi pamoja na kuboreasha mazingira  ya utoaji huduma za afya nchini" Amesema  Majaliwa.

Aidha ameipongeza kampuni ya Amsons Group kwa kujitolea kujenga wodi hiyo  na kuahidi kusema serikali inathamini mchango  wake na itaendelea kuipa ushirikiana kampuni hiyo.
Pia  aliutaka uongoziwa hospitali ya Amana,  kuanisha nyumba zinazoizunguka hospitali hiyo ili kuangalia  upanuzi  wake.

Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda, alisema kampuni ya Amsons Group mbali na ujenzi huo pia itajenga majengo mengine mawili katika hospitali za Temeke na Mwananyamala.

“Wodi hii  linauwezo wa kuchukua wagonjwa zaidi ya 100 ni muhimu kwaajili ya wanawake ambao walikuwa wanapata taabu ya kulala chini au watatu katika kitanda kimoja baada ya kujifungua,”alisema Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages