Msanii wa muziki, Vanessa Mdee amedai ametumia gharama kubwa katika kuiandaa albamu yake mpya MoneyMonday.
Muimbaji huyo amesema kuwa albamu ya MoneyMonday mpaka kukamilika imemgharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 100.
“Nimetumia fedha nyingi lakini kwangu sioni tatizo lolote, niliangalia
zaidi jinsi gani watu watatambua Vanessa kafika wapi katika kukua
kimuziki, fedha hiyo nililipa idara zote kuanzia wasanii walioshiriki
matangazo, video nk na bado naendelea kutoa kwa kuwa matangazo bado
yanaendelea ,” Vanessa aliuambia mtandao wa Dar 24.
Ameongezea kuwa hajutii matumizi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa
kuwa lengo lake hasa ni kutoa kazi itakayomwongezea heshima kwenye
muziki wake sambamba na kuhakikisha inawifikia watu wa aina zote.
Hivi karibuni Vanesa ameachia albamu yake katika ukumbi wa Mlimani City.
Vanessa ni kati ya wasanii wachache ambao wanajaribu kurudisha utamaduni
wa kutengeneza Albamu katika muziki wa Bongo fleva jambo ambalo kwa
siku za nyuma limekuwa likififia na kupotea.
Naye Diamond Platinum anajipanga kuaachia albamu yake ya Mtoto wa
Tandale ambapo juzi alitaja baadhi ya sababu zilizomfanya acheleweshe
kutoka kwa albamu hiyo.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, February 7, 2018
Vanessa Mdee ametumia zaidi ya milioni 100 kuandaa albamu yake mpya ‘MoneyMonday’
Tags
BURUDANI#
Share This
About kilole mzee
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment