A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 7, 2018

Kauli ya Msajigwa kuhusu mechi ya Simba, Azam

Kocha Msaidizi wa klabu ya Yanga, Shadrack Msajigwa ameogopa kuongelea mechi ya watani wao wa jadi Simba dhidi ya Azam FC, kwa kudai wao wanajiangalia wenyewe na wala sio timu nyingine japokuwa lazima uwepo ushindani kwenye ligi.

Msajigwa amebainisha hayo baada ya kuulizwa swali kuhusiana na mchezo wa leo, ambao ni muendelezo wa mashindano ya 'VPL' utakaochapwa katika dimba la Taifa kwamba angependa timu gani itoke na ushindi dhidi ya mwenzake jambo ambalo kwake ameshindwa kulitolea majibu ya uwazi.

"Sisi mara zote tunajiangalia wenyewe japokuwa lazima kuwepo na ushindani lakini zile ni timu zinashindana na zipo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kama zilivyo nyingine, kwa hiyo tunawaachia wao. Mtu ambaye atakaepoteza mchezo wa leo anazidi kujididimiza na nasi ndio tunasonga mbele", amesema Msajigwa.

Pamoja na hayo, Msajigwa amesema "kama tutakuwa tunaendelea kupata matokeo haya kila mechi na wenzetu wakipata mabaya basi itakuwa neema kwetu ila sisi tunawatakia mchezo mwema".

Kutokana na ushindi waliyoyapata jana (Jumanne) Yanga wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji wameweza kuishusha Azam katika msimamo wa Ligi na kukamata nafasi ya pili kwa alama 34, huku tofauti kati yake na vinara Simba ikiwa pointi 4 pekee.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages