A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, February 4, 2018

Shinikizo lakumtaka rais Zuma kujiuzulu lazidi kuongezeka


Shinikizo linaongezeka dhidi ya rais Jacob Zuma Afrika kusini kujiuzulu, huku maafisa wakuu kutoka chama tawala ANC wakitarajiwa kukutana naye Jumapili kujadili mustakabali wake.

Rais Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka kumtimua madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maafisa wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu "ugavi wa uongozi" ndani ya chama.

Lakini nyuma ya kauli hiyo nyepesi - vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo.

Rais Zuma bado yupo madarakani, lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu tena wa ANC.

Waendesha mashtaka wakakamavu sasa wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu.

Wengi ndani ya ANC wanamtaka rais huyo ajiuzulu hara iwezekanavyo, ili waweze kulenga kujenga upya sifa ya chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani.

Lakini kuna taarifa kwamba Zuma anajikita kisawasawa.

Anatarajiwa kulihotubia bunge wiki ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza kuwa hastahili kusalia kama rais.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama na serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages