Kutokana na idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameamua kuongeza siku moja hadi kesho ili kuhakikisha wananchi wote waliofika wanasikilizwa na kuhudumiwa.
Akiongea kwa niaba ya RC Makonda, Mwenasheria wa ofisi ya mkoa wa Dar es salaam Fabiola Mwingira amesema idadi ya wananchi waliojitokeza ni kubwa tofauti na matarajio lakini wamejitaida hadi sasa zaidi ya Wananchi 3,000 wamepatiwa huduma.
RC Makonda pia amewatangazia Wananchi wote waliosikilizwa na wanasheria kufika ukumbi wa Diamond Jubilee ifikapo Tarehe 10 February kuanzia Saa moja Asubuhi kwaajili ya kupatiwa mrejesho.
Taarifa za kuongezwa kwa muda zimepokelewa kwa shangwe na Wananchi ambapo wamemsifu RC Makonda kwa kutanguliza Utu mbele kwa kuhakikisha wanyonge wanaipata haki yao waliyotaabika kuitafuta kwa miaka mingi.
HONGERA RC MAKONDA KWA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS MAGUFULI.
No comments:
Post a Comment