Wema na Diamond.
MWANAMITINDO maarufu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, ambaye awali
alikuwa meneja wa staa mkubwa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, amepata
kigugumizi kikubwa cha kuelezea kuhusu mrembo huyo kurejesha penzi lake
na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza na Amani, Kadinda alipata kigugumizi hicho baada ya kuulizwa
endapo mastaa hao watarudisha mapenzi atalichukuliaje suala hilo ambapo
alishindwa kufafanua badala yake aliishia kuguna na kuomba kama kuna
swali lingine aulizwe.
Martin Kadinda.
“Jamani mimi siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo na hata sijui
nianzie wapi kuzungumza lakini kama kuna ishu nyingine yoyote
nitazungumza kwa mapana yote lakini siyo hilo hata kidogo kwa kweli,”
alisema Kadinda.
Wema anatajwatajwa kurudisha ‘majeshi’ kwa Diamond baada ya hivi
karibuni, mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza
kummwaga Diamond.
No comments:
Post a Comment