Ndege ya kivita ya Syria imeshambuliwa na kuangushwa Idlib nchini Syria.
Kwa mujibu wa habari,ndege hiyo ya kivita ya Su-25 ilishambuliwa na kuanguka.
Rubani wa ndege hiyo aliweza kujiokoa kwa kuruka kabla ya ndege hiyo kuangushwa lakini baadae alipoteza maisha yake.
Rubani huyo alipoteza maisha baada ya kuingia katika eneo linalotawaliwa na El Nusra.
Baada ya tukio hilo Urusi imefanya mashambulizi ya anga na kuwaangamiza watu 30 kutoka katika kundi hilo.
No comments:
Post a Comment