Muimbaji Lulu Diva amedai kuwashangaa watu wanaomsema kwamba amebadili muonekano kwa kutumia dawa za kichina na kusema kwamba yeye atakuwa siyo mtu wa kwanza kufanya hivyo na kwamba hata mwimbaji maarufu duniani Michael Jackson aliwahi kujibadilisha.
Akiwa mbele ya kamera za eNEWZ Lulu Diva amesema kwamba kila mtu ana uhuru wa kufanya chochote kwenye mwili wake hivyo kama watu wanadhani kwamba anatumia mchina wako sahihi ingawa yeye anaamini kuwa maisha anayoishi sasa ndiyo yanamfanya muonekano wake wa mwili kubadilika na kuvutia.
"Jamani yani mtu usifanye kitu watu lazima waongee mimi huu mwili ni wangu na ukuaji tu jamani napata mashabiki wazuri na wapya kila siku nakula vizuri naishi pazuri ndio maana hata nakuwa hivi na kariakoo huwezi pata sexy look kama yangu jamani hebu watu waache kuongea. Na hata kama nimebadili mbona nitakuwa siyo wa kwanza Michael Jackson alibadilisha kuanzia muonekano wa rangi mpaka viungo," Lulu Diva
Akiendelea kujitetea Lulu Diva amesema kwamba kwa sasa anafanya mazoezi ambayo yamesababishia umbo lake kuonekana vyema, huku akiongeza kwamba anazidi kukua na viungo vimeanza kujipanga kukaa sehemu sahihi za mwili.
Lulu Diva kwa sasa anafanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina la Mazoea .
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, February 3, 2018
Lulu Diva kufata nyayo za Michael Jackson?
Tags
BURUDANI#
Share This
About kilole mzee
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment