Mwenyekiti wa Muda wa Asasi ya kiraia ya Legal Services Facilities (LSF) Dkt. Benson Bani , akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya LSF Bw. Kees Groenendijk akitoa mada yake ambapo alizungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelezea malengo, mambo mbalimbali yaliyofanyika kwa mwaka 2017 pamoja na mwelekeo kwa mwaka 2018, wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Meneja Miradi wa LSF Bw.Ramadhani masele akielezea kiundani juu ya utendaji , mrejesho na nini kifanyike wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Baadhi ya wakurugenzi na wajumbe wa Bodi za ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakitoa maoni mbalimbali wakati wa warsha hiyo
Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka LSF Bi. Saada Mkangwa akitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa taarifa za wanufaika wa ruzuku.
Mkurugenzi wa miradi wa LSF Bi. Scholastica Julla akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Makundi mbalimbali ya ya wakurugenzi pamoja na wajumbe wa bodi za wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakijadili mambo mbalimbali na namna watakavyofanya kazi na LSF kwa mwaka 2018.
Wawakilishi katika makundi wakitoa mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria, ambapo wote walionesha kuwa watafanya kazi zao kwa weredi zaidi kwa mwaka 2018
Meneja wa ufuatiliaji na matokeo kutoka LSF Bw. Said Chitung akielezea mambo mbalimbali pamoja na malengo ya LSF kufikia 2021 wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Wakurugenzi na wajumbe wa bodi wakati wakiendelea kufuatilia mambo mbalimbali ya warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria iliyofanyika jijini Dar es salaam.Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania
No comments:
Post a Comment