Jamii inayofuga mbwa imekumbushwa kihakikisha inatimiza siha za wanyama Hao ikiwemo kuwapatia chakula,matibabu pamoja na kuacha kuwafungia kwa muda mrefu kwenye mabanda.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa umoja wa wadau wa mbwa wakati wa akitoa taarifa juu ya uzinduzi wa Chama cha wafuga mbwa utakaofanyika siku ya February 2 mwaka huu katika ukumbi wa Leaders Club jijini Dar es salaam.
Dr.Sinare amesema kwamba wafugaji wengi wa mbwa wamekua wakikiuka haki za wanyama wakufugwa,ambapo Mbwa wamekua wakifungiwa muda mrefu kwenye banda,huku wakiwapatia chakula kisicho ubora,pamoja na kushindwa kuwatibu.
Awali Akizungumza uzinduzi huo Dr.Sinare amesema kwamba mgeni rasmi atakua Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro,ikiwa lengo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali na wafugaji wa mbwa kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment