Bondia Francis Cheka akiwa amesimama Mbele ya Jengo la Ofisi ya TAMOFA maara baada ya Kupewa Ubalozi wa Chama Hicho Mkoani Mtwara.
Chama cha Urafiki wa Wananchi wa Nchi ya Tanzania Na Msumbiji TAMOFA Kimempa Ubalozi Bondia wa Kimataifa Francis Cheka Ili kuweza Kutangaza Chama Hicho kwa lengo la Kujipatia wafadhili ndani na nje ya nchi.
Akiongea mara baada ya makabidhiano ya kadi ya ubalozi Mkoani Mtwara Francis Cheka anasema Urafiki wa msumbiji na Tanzania Umekuwa wa Muda Mrefu na hivyo kuhamasisha wananchii kujiunga na chama hicho hasa wale wanaofanya safari katika nchi hizo mbili.
Hamza Lichete ni katibu mwenezi wa TAMOFA anasema kazi kubwa ya chama hicho ni kuimarisha Mahusiano pamoja na kulinda Umoja kati ya nchi hizi mbili kwa lengo la kuimarisha uchumi pamoja na amani.
Cheka ambaye kwa sasa anaishi Mkoani Mtwara amezaliwa Nchini Msumbiji lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akiitangaza Tanzania katika mapambano mbalimbali ya Kimataifa ambayo yamempatia umaarufu yeye pamoja Na Nchi ya Tanzania
No comments:
Post a Comment