Raia huyo wa Ufaransa alitoa mifano nchini ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Uhispania.
PSG iko pointi 11 juu katika ligi ya kwanza , Bayern Munich iko pointi 16 juu katika ligi ya Bundesliga na Manchester City ipo pointi 15 juu ya jedwali la ligi ya Uingereza.
Wenger amesema kuwa ni wazi kwamba hakuna tena utabiri .
Aliongezea: Unapozitazama ligi tano barani Ulaya mnamo mwezi Disemba , unaweza kujua ni timu gani zitakazoshinda ligi zao.
- Wenger amtetea Sanchez kuhusu kupimwa
- Jinsi klabu za EPL zilivyogharamika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho
Hiyo inamaanisha kwamba kunakitu hakiko sawa katika mchezo huu. Utajiri mkubwa wa baadhi ya timu unaharibu ushindani uliokuwepo.
Nchini Uhispania, Barcelona ina pointi 11 juu ya jedwali la ligi dhidi ya Athletico Madrid huku mabingwa watetezi Real Madrid wakikumbwa na msimu mgumu, wako pointi 19 nyuma ya Barca katika nafasi ya nne.
Ligi nyengine ambayo inatamatisha ligi tano bora za Ulaya ni Itali ambapo Napoli wapo pointi moja mbele ya Juventus ambao wameshinda taji hilo kwa misimu sita mfululizo.
Wenger alikuwa akizungumza siku mbili baada ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Uingereza lililovunja rekodi kwa matumizi.
Klabu za Uingereza zilitumia £150m siku ya Jumatano ,katika siku ya mwisho ya uhamisho na hivyobasi kujumlisha matumizi hayo kwa mwezi kufika £430m.
Kufikia mwisho wa dirisha la uhamisho mnamo mwezi Septemba , Wenger alisema kuwa sheria ya Uefa ya Fair Play ilioanzishwa ili kukabiliana na ubabe wa kifedha inafaa kufutwa kwa kuwa klabu haziiheshimu.
Mabingwa wa Ufaransa PSG waliweza kulipa mara mbili ya ada ya uhamisho uliovunja rekodi wakati walipomnunua Neymar kutoka Barcelona mwisho wa msimu uliopita mbali na kumsajili Kylian Mbappe kwa mkopo ambao utamwezesha kujiunga na klabu hiyo kwa dau la £165.7m mwisho wa msimu huu.
Manchester City walishutumiwa kwa kutumia vibaya utajiri wao na rais wa ligi ya Uhispania Javier Tebas ambaye pia alisema kwamba PSG ilikuwa ikiucheka mfumo uliowekwa kutokana na ununuzi wao wa mwisho wa msimu.
Mwezi Januari matumizi ya klabu za Uingereza yalipiku yale ya wenzao wa Ulaya licha ya Barcelona kulipa dau la juu wakati walipomnunua Phillipe Coutinho kutoka Liverpool kwa thamani ya £142m.
Ligi ya Bundesliga imekuwa ikitawaliwa na Bayern katika miaka ya hivi karibuni wakiwa wameshinda mataji 12 kati ya 18 ikiwemo mataji matano yaliopita mfululizo.
Ni mara moja katika misimu 13 iliopita ambapo taji la Uhispania limeshindwa na klabu nyengine isipokuwa Real Madrid na Barcelona , ambapo Atletico Madrid ilishinda 2014 .
Barca imelishinda taji hilo mara nane katika kipindi hicho huku Madrid ikilishinda mara nne.
Nchini Itali , Juventus imeshinda taji la Serie A kwa kipindi cha misimu sita iliopita mfululizo huku Inter Milan ikishinda mataji matano kati ya 2006-2010.
Nchini Ufaransa kulikuwa na washindi wa mataji sita tofauti kati ya 2007-08 na 2012-13 lakini PSG imeshinda ligi hiyo katika misimu minne kati ya tano iliopita.
Kati ya 2002 na 2008 , Lyon ilishinda mataji saba ya ligi ya daraja la kwanza mfululizo.
Katika Ligi ya Uingereza, ni klabu nne - Chelsea, Manchester City na Leicester ambazo zimeshinda ligi katika misimu 12 iliopita.
Tangu ianzishwa 1992 , ni klabu sita ambazo zimeshinda huku Blackburn Rovers na Arsenal zikiwa klabu nyengine mbili zilizoshinda taji hilo.
No comments:
Post a Comment