Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imezindua
Promosheni ya Shinda na Smatika kupitia kifurushi cha yatosha chenye lengo la
kuwazawadia Wateja watakaojiunga na huduma ya Bando za Yatosha Smatika
Intaneti.
Akiongea leo katika uzinduzi wa Promosheni hiyo, Mkurugenzi
wa Masoko Airtel Tanzania ISACK NCHUNDA
amesema promosheni hiyo inalenga wateja wa Intaneti ambao watanunua kifurushi
cha bando ya Yatosha SMATIKA Intaneti,ambapo
watanufaika na huduma hiyo hivyo ametoa
hamasa kwa wateja kuendelea kutumia huduma za intaneti amabazo ni nafuu na
rahisi.
Amesma huduma ya bando nafuu za Yatosha SMATIKA Intaneti
ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana zilizolenga kutoa uhuru kwa mteja wa
Airtel kote nchini kujiunga banddo la Intaneti KABAMBE wkati wowote.
"Mteja wa Airtel anaweza kunufaika na Yatosha SMATIKA Internet
kwa gharama nafuu zaidi ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40,vilevile ofa
hii inamwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku
tatu mfululizo kwa shilingi elifu mbili pekee"Amesema Nchunda.
Nchunda amesema kuwa promosheni hiyo itakuwa ya uwazi na wateja hawahitaji kujisajili ila
anachotakiwa kufanya ni kuwa na laini ya Airtel na kuweza kujiunga na kifurushi
hicho kwa kupiga *149*99# na kuweza kuchagua kifurushi.
"Mteja wetu anachotakiwa kufanya ni kuwa na laini ya
Airtel tu halafu atajiunga kwenye kifurushi cha yatosha Smatika Intaneti kwa
kupiga *149*99# halafu unachagua namba 5 Yatosha Smatika Intaneti,hapo utanunua
bando ya siku au ya mwezi kadri uwezavyo na kuwa mmoja wa washndi wa zawadi
zetu kabambe"Amesema mkurugenzi wa
Masoko Airtel Tanzania.
"Promosheni ya Sinda na Yatosha SMATIKA Inteneti
itadumu kwa siku 30huku kukiwa na droo taatu kila wiki yaani Jumatatu,ajumatano
na Ijumaa,ambapo droo za kila siku wateja 1000 wataweza kujishindia bando ya
Intaneti yenye 1GB kila
mmoja wakati kweye droo kubwa watakuwepo washindi 10 ambao watano kati yao
watajishindia simu za Smatiphone na watano watajishindia moden"amesema
Nchunda.
No comments:
Post a Comment