RC Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March
13 siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika
likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa
wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.
RC Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa
walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa
kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto lakini kupitia jengo
hilo vifo vinaenda kupungua.
Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa
Jengo hilo ambapo inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia
1,500 hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya
Upasuaji.
No comments:
Post a Comment