Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya Ziara katika kampuni ya Dar
Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi
na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo
ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa
yameshakamilika na kukabidhiwa.
Akizungumza
mara baadaya kutembelea Kampuni inayofanya Ukarabati wa magari hayo Makonda
amesema kuwa zoezi la Ukarabati hayo litasaidia kuboresha mazingira ya
kazi kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuwa kazi ya Ulinzi na Usalama ni wa
Raia na linahitaji mazingira rafiki ya kazi.
Aidha
Makonda amedhibitisha kulidhishwa na kasi ya ukarabati wa mabasi hayo ambapo
amekishukuru kiwanda cha Dar Coach Ltd kwa uzalendo wa kujitolea kukarabati
Magari hayo ili kuongeza ufanisi katika vyombo vya ulinzi na usalama.
"Kama
mnavyokumbuka Magari haya ni yale yaliyokuwa Chakavu ambapo kwasasa yapo katika
hatua ya mwisho kukamilika ambapo yatafungwa vifaa vya kisasa ikiwemo AC, Chaji
ya Simu, TV, Viti, Bodi mpya, Taa, Side mirrors, Tairi, Vioo huku baadhi
zikiwekewa Vyoo vya Ndani kwa lengo la kuweka mazingira Rafiki kwa vyombo vyetu
vya ulinzi na usalama" amesema
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Coach LTD ambayo imejitolea
kufanya Ukarabati huo Manmeet Lal amesema kuwa zoezi hilo ni katika kuunga
mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha Ulinzi na usalama wa Raia na
mali zao kwa ujumla. Pia amemhakikishia Rc makonda hadi mwishoni mwa mwezi huu
kumkabidhi magari matano ambayo yameshakamilika.
Hata
hivyo kwa upande wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar ea salaam Lazaro
Mambosasa,amemshukuru Rc makonda kwa hatua aliyoichukua kusaidia vyombo vya
ulinzi na usalama kupitia wadau wake kusaidia kukarabati mabasi hayo ambayo
yatasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishikana mikono na Meneja Mauzo wa Kampuni
ya Babasi ya Scania Hanif Ally,walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda
kufanya ziara kwenye Kampuni ya Dar
Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi
na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo
ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa
yameshakamilika na kukabidhiwa mwengine (kulia) ni mmoja wa Maofisa wa kampuni ya Scania Deogratias Kabeho.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul MakondaA akishikana mikono na Mmoja wa Maofisa wa Kampuni ya Babasi ya Scania
Deogratias Kabeho walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya
ziara kwenye Kampuni ya Dar Coach LTD,
na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama
ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa
hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na
kukabidhiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Dar Coach Ltd Manmeet Lal (Sunny) wakati Mkuuwa Mkoa
alipokwenda kufanya ziara kwenye Kampuni
hiyo na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na
Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo
ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa
yameshakamilika na kukabidhiwa.
Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea
kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya Dar Coach.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
No comments:
Post a Comment