Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa
mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi
wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula
pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea
watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa, kushoto ni Mkurugenza
wa Fedha wa Taasisi hiyo, Oswald Urassa.
Mkurugenzi
wa Taasisi inayotoa Mikopo kwa Mabenki na Taasisi nyingine
za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar
Mgaya (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa
vyakula pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu yenye thamani ya shilingi
Milion 2 kwa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,kushoto
ni Mlezi Mkuu wa Kituo hicho Elias Mwakalukwa wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine
za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili
kushoto) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas kwa mwakilishi wa Wanafunzi wa
Kituo hicho. Picha na Brian peter
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TMRC
YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KIWALANI
13, DESEMBA 2017 - (DAR
ES SALAAM), Kampuni ya Tanzania Mortgage
Refinance Company Limited (TMRC), imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye
thamani ya Shilingi Milioni Mbili (Shilingi 2,000,000) kwa Kituo cha Watoto
yatima cha Kiwalani (Kiwalani Orphanage Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC,
Bw. Oscar P. Mgaya kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji Elias
Mwakalukwa -, katika ghafla iliyofanyika kwenye Kituo hicho kilichopo jijini
Dar es Salaam.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho cha watoto
yatima ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage sabuni
za kufulia na kuogea, sukari , chumvi,
dawa za meno, majani, kalamu na madaftari
“Kwa upendo wetu wa dhati kabisa tumeona umuhimu wa kushiriki
pamoja na watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu,
katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.
Bw. Mgaya, alisema kuwa taasisi yake imeamua kujumuika na
watoto hawa yatima katika kuelekea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kutoa
zawadi mbalimbali za vyakula kama njia ya kuwafanya wajisikie furaha.
Hata hivyo, Mtendaji Mkuu huyo, amezitaka taasisi nyingine na
watu binafsi kujitoa kwa dhati kuwasaidia watoto walioko maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo
hicho, Mchungaji Elias Mwakalukwa,
ameishukuru TMRC, kwa msaada huo na ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wao.
“Tunaishukuru sana TMRC, ninyi
mmeonyesha mfano na hakika mmeonyesha upendo wa dhati kwa watoto hawa. Niziombe
taasisi nyingine kuchukua mfano huu uliofanywa na taasisi yenu,” Mchungaji Elias Mwakalukwa alisema.
Aliongeza kuwa uhitaji wa misaada kwa
kituo chake ni mkubwa, lakini taasisi yao inapata faraja kupata wadau wanao ona
umuhimu wa kusaidia watoto hao yatima.
No comments:
Post a Comment