Mganga mkuu wa Manispaa ya kinondoni Dk. Festo Dugange akiungumza.
Viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa waliofika katika.zoezi hill la kukabidhiwa jengo kwa ajili ya ahanati
Hili ndilo jengo ambalo linatarajiwa kuwa kituo hicho
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amemwomba mganga mkuu kuharakisha ukarabati wa Jengo lililonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kituo cha Afya cha Kigogo jijini Dar es Salaam, litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 46 kwa lengo la kusaidia matibabu kwa wananchi haraka ipasavyo.
Sitta ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhiwa hati ya Jengo hilo ambalo kwa sasa ni kituo cha Afya Manispaa ya konondoni kata ya kigogo, lililonunuliwa na serikali kutoka Dogodogo Center Street Children Trust(Caring for our Childen) lililogharimu kiasi cha shilingi milioni 400.
Amesema mahitaji katika sekta ya afya ni mkubwa sana na hivyo serikali inajtahidi kupunguza bajeti kwenye vitu vingine inawekeza kwenye mambo kama haya ya kijamii kwani wananchi wanauhitaji mkubwa katika sekta ya Afya .
"Mahitaji ya wananchi wetu kwenye sekta ya afya bado ni makubwa sana ,lakini kigumu zaidi kwenye manispaa yetu ya Kinondoni,Na kigogo ikiwa na kituo cha afya itahudumia watu wengi kutoka sehemu tofauti tofauti na tunayafanya haya kwa wananchi wetu wote,katika kuwatekelezea mahitaji yenu muhimu ambapo afya ni namba moja kwa jamii.Amesema Meya wa Kinondoni.
Aidha amesema katika manispaa hiyo wanategemea kila mtaa uwe na Zahanati na kila Kata kuwe na kituo cha afya ili kufanikisha hayo amesema wanategemea kujenga hospitali ya kisasa Magwipande lengo likiwa ni kupunguza msongamano katika hospitali ya Mwananyamala,sambamba na kujenga hospitali ya Apolo India itakayohudumia wagonjwa wanaokwenda kutibiwa huko.
"Tumefanya jambo kubwa sana,ni mategemeo yetu kila Mtaa uwe na Zahanati na kila kata kuweze kuwa na Kituo cha Afya, ingawa tuna upungufu wa Zahanati 84, pamoja na vituo vya afya 18 na tumeanza mazungumzo ya kujenga hospitali ya Apolo ya India yetu itakayosaidia kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje na kuweza kutbiwa hapa hapa nchini na pia tunatarajia kujenga hospitali ya kisasa kabisa Mgwipande katika manispaa yetu itakayopunguza msongamano katika hospitali yetu ya Mwananyamala" Amesema Sitta.
Kwa upande wake Naibu Meya ambaye pia ni Diwani kata ya kigogo Mangalu Manyama,ameishukuru Serikali katika kufanikisha kununuliwa kwa Jengo hilo ambapo litakarabatiwa na kuwasaidia wakazi wa kata ya kigogo kupata matibabu katika kituo hicho.
Mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni Dk. Festo Dugange amesema katika halmashauri hiyo inatekeleza Adhima ya serikali kujenga Zahanati pamoja na Vitio vya Afya ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreka katika jamii ambapo majengo waliyonunua kutoka Dogodogo Center itasidia wananchi kupata huduma kwa haraka Zaidi kutoka katika kituo cha Afya kwani Katika Zahanati ya kigogo inahudumia watu 66,654 kutokana na ufinyu wa majengo ya huduma za afya.
”Majengo haya na eneo hili lililonunuliwa kutoka Dogodogo Center itasaidia sana kupunguza msongamano wa Wagonjwa katika Zahanati ya KIgogo kimsingi Zahanati inatakiwa isihudumie wagonjwa zaidi ya 5,000 lakini zahanati yetu inawahudumia wakazi wapatao 66,654 zaidi ya mara kumi na mbili ya uwezo wa zahanati" Amesema Dk. Dugange.
No comments:
Post a Comment