Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina
Masenza alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukakua shughuli
mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni.
Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili
kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa
uchumi wa viwanda.
Naibu
Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua baadhi ya
vifungashio vya asali alipotembelea shamba la miti Sao Hill kwa ajili ya
kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa
hivi karibuni. Asali inayozalishwa na shamba hilo imefanyiwa vipimo
nchini Ujerumani na kugundulika kuwa ni bidhaa bora isiyo na viambata
vya kemikali ya aina yeyote. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na Afisa Ufugaji Nyuki wa shamba hilo, Said Abubakar.
Meneja
wa shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akimueleza Mhe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) kuhusu moto
uliovamia hekta 77 za shamba hilo na hatua zilizochukuliwa kuudhibiti
alipotembelea kukakua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa hivi
karibuni, alisema moto huo uliozuka hivi karibuni ulianzia kwenye
mashamba ya wananchi haukuwa na madhara makubwa.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet
Hasunga kuhusu utafiti unaofanywa na shamba hilo kwa kushirikiana na
Kampuni ya Art International kuhusu uvunaji wa utomvu kwa ajili ya
kutengeneza madawa mbalimbali, bazooka (chewing gums) na ‘gel’ kwa ajili
ya kujiongezea kipato alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli
mbalimbali hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mhe. Jamhuri David.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet
Hasunga (hayupo pichani) kuhusu njia mpya ya kuzalisha mbegu za miti
kwa njia ya vikonyo ili kuongeza zaidi uzalishaji alipotembelea shamba
hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi karibuni. Aliagiza uongozi wa
shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji
makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina
Masenza (wa pili kulia) alipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha
Ismila kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho mkoani
Iringa hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina
Masenza (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya
Kale, Laurent Nampunju (kulia) kuhusu fuvu la Chifu Mkwawa alipotembelea
Makumbusho ya chifu huyo kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na
kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga mkoani Iringa hivi karibuni.
Jengo la Makumbusho ya Mkwawa ambalo lipo ndani ya Kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga Mkoani Iringa.
Picha ya Chifu Mkwawa ambayo inapatikana katika makumbusho hayo.
Muonekano wa fuvu la Chifu Mkwawa ambalo pia linapatikana katika makumbusho hayo. (Picha na Hamza Temba - WMU)
No comments:
Post a Comment