Dar es Salaam, Tarehe 31 Oktoba,
2017 - Kampuni ya Uber ina furaha kuwatangazia madereva wake wote kwamba
imezindua vipengele vipya vyenye uwezo mkubwa vitakavyowasaidia madereva kutoka
kanda ya Afrika Mashariki kuwa na uhuru wa kuchagua maeneo, muda na namna
wangependa kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber. Halikadhalika Uber imeongeza
mara dufu uwezo wa programu yake na kuifanyia maboresho makubwa.
Vipengele hivi vipya vinakuja
baada ya zana ya Kuchati Ndani ya Programu Iliyozinduliwa hivi karibuni,
kipengele kinachowasaidia madereva na wasafiri kuwasiliana kwa kutumia programu
ya Uber bila kuonesha namba zao za simu wanapotaka kuwasiliana.
Meneja Msimamizi wa Uber Nchini
Tanzania, Alfred Msemo, anaelezea, "Siku zote sis hufanyia kazi maoni ya
madereva wetu ambayo hutusaidia katika kuboresha na kuimarisha wigo wa madereva
wanaotumia mfumo wetu. Madereva wanaotumia mifumo yetu wameeleza wazi kuhusu
kile wanachotaka na tumefanyia kazi maoni yao, kwa hiyo tutazindua bidhaa
ambazo zitasaidia kutafuta mwafaka katika sehemu tatu kuu: kuwapa madereva
uhuru zaidi hasa namna wangependa kutumia mfumo wa Uber, kutumia teknnolojia
kuwaondoleaa kero zozote wanazopata kazini, pamoja na kuimarisha usalama.”
Kampuni ya Uber itaanza kwa
kuzindua bidhaa kadhaa ambazo madereva wameomba:
Kuonesha Safari Yangu ya Dereva: Tayari Uber ina njia ambayo
msafiri anaweza kuwaonesha watu wanaotaka alipofika kwenye safari yao yake,
sasa kipengele cha Kuonesha Safari Yangu kinatoa nafasi kwa madereva kuonesha
watu wa karibu maelezo ya safari yao, bila kuingilia faragha ya msafiri au
kutoa taarifa ya kibinafsi au vituo vya kuchukua na kushusha abiria.
Kituo na Muda wa Kuwasili: Sasa madereva wanaweza kuweka
muda wanaotaka kuwasili mahali wanakoenda wakati wowote kwa kutumia kipengele
cha Muda wa Kuwasili. Madereva wakiweka kituo na muda wa kuwasili,
wanapoendelea na shughuli zao za kawaida programu itawakumbusha muda wa kuanza
safari ukifika. Muda ukifika wataunganishwa na msafiri aliyeita gari kwenye
barabara hiyo. Kipengele hiki kinawapa uhuru zaidi wa kujisimamia sambamba na
kupata pesa zaidi wanapokuwa njiani kuelekea kituo wanachotaka.
Arifa ya safari ndefu: Madereva watapata
taarifa mapema itakayowajulisha kuhusu safari ya mwendo mrefu, hii ina maana
kwamba madereva watajua mapema ikitokea kwamba safari itachukua dakika 45 au
zaidi, ili wafanye maandalizi ya kutosha.
Kulinda Ukadiriaji: Wakati mwingine wasafiri
wanaweza kukadiria safari vibaya kutokana na sababu ambazo sio kosa la dereva
kama vile hitlafu kwenye programu ya Uber. Sera mpya ya kumkadiria dereva,
ukadiriaji wa aina hii hautajumuishwa kwenye jumla ya ukadiriaji wa dereva.
Bado kampuni ya Uber itandelea kupokea maoni yatakayosaidia kuboresha huduma
zake lakini hayataathiri wastani wa ukadiriaji wa dereva.
Kitufe cha 'Hapana': Kipengele hiki
kinawapa madereva uhuru wa kukataa safari bila hofu ya kwamba itaathiri mapato
yao. Kwa sasa, madereva wanaweza kuthibitisha na kukubali safari au wasubirie
muda wa ombi la usafiri uishe. Kipengele hiki kipya, cha kitufe cha 'hapana',
kinawapa madereva uwezo wa kukataa safari mara moja - ni habari njema kwa
wasafiri pia kwa sababu ombi litatumwa kwa dereva mwingine haraka hivyo
hatapoteza muda mwingi akisubiria gari.
Ni nini tafsiri yake kwa
madereva? Msemo anafafanua, “Fatuma Mdee anapofungua pprogramu na kuanza
kukubali maombi ya wasafiri, anaweza kutumia kipengele cha “Onesha Safari
Yangu” kumtumia mume wake maelezo ya safari yake. Maelezo haya ni kama vile
mahali alikofika kwenye ramani. Ana uwezo wa kuanza kumwonesha mume wake na
watu wengine lakini anaweza pia kuacha kuwaonesha maelezo ya safari yake muda
wowote, na wanaweza kufuatilia mahali amefika bila ugumu wowote kwenye ramani
kwa kutumia maelezo yake ya namba ya simu na namba pleti ya gari. ”
"Au kwa mfano, dereva Omar
Mohammed, ambaye ni baba wa watoto watatu na anatumia programu ya Uber kumpa
uhuru wa kusimamia maisha yake. Kitufe hiki kipya cha "Hapana", sasa
kinawapa madereva kama Omar uhuru zaidi wa kusimamia safari kwa sababu
kipengele hiki kinampa uwezo wa kukataa safari mara moja bila wasiwasi wowote
wa mapato yake kupungua. Hii ni habari njema kwa wasafiri pia kwa sbabu ombi la
usaifiri litatumwa moja kwa moja kwenda kwa dereva mwingine bila kupoteza muda
wowote.
"Tunajituma kila siku
kutumia uwezo wetu wa teknolojia na ofa zetu za madereva ili kuwajengea
madereva mazingira rafiki na wafurahie kazi yao wanapotumia mfumo wa Uber.
Tunaamini kwamba vipengele hivi vitaimarisha sio tu wigo wa madereva bali
maisha yo pia. "Amehitimisha Bw. Msemo.
Lakini huu ni mwanzo tu -
tumekusudia kuyapa kipaumbele maslahi ya dereva katika mkakati wa Uber, Uber
itaendelea kujituma ili kuimarisha wigo wa madereva wanaotumia programu yetu.
Maboresho haya si ya vipengele tu - ni sehemu ya mkakati endelevu, na Uber ina
furaha kubwa kutumia uwezo wake wa kiteknolojia ili kuimairsha na kubadilisha
wigo wa madereva 1,000 wanaotumia mfumo wa Uber kila wiki.
Kuhusu Uber
Kampuni ya Uber imedhamiria
kuwasaidia watu mahali popote walipo kupata usafiri kwa kutumia simu zao.
Kampuni hii ilianza mwaka 2009 kutafuta mwafaka wa changamoto za usafiri -
msafiri anawezaje kupata usafiri kwa kutumia simu? Miaka sita sasa tumetekeleza
zaidi ya safari bilioni mbili, sasa tunakabiliana na changamoto kubwa zaidi:
kupunguza foleni na uchafuzi wa mazingira katika miji yetu kwa kutumia magari
machache kusafirisha watu.
Sasa mtandao wa Uber unapatikana
katika miji isiyopungua 600 katika zaidi ya nchi 75 katika mabara 6. Watumiaji
wanatakiwa wajipatie programu ya Uber kwenye simu za Android, iPhone,
Blackberry 7 bila malipo ili waweze kuita usaifiri, au wajiandikishe kutumia
Uber kwenye www.uber.com/go. Kama una maswali yoyote tafadhali tembelea
www.uber.com
Kwa habari zaidi wasiliana na:
Bi. Janet C. Kemboi - Mawasiliano
- Afrika Mashariki
Tel: +254726390190
Barua pepe: jkemboi@uber.com
No comments:
Post a Comment