Balozi
wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akihutubia katika mkutano
wa Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika Taifa la
China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Watanzania wanaosoma nchini China (TASAFIC) Bw.
Remidius Emmanuel akizungumza katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika
mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Afisa
Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China (Mwambata wa Elimu) Bw.
Lusekelo Gwassa Akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa TASAFIC kwa
Mwaka 2017.
Baadhi
ya Watanzania wanaosoma nchini China waliohudhuria Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Jumuiya ya Watanzania wanaosoma katika Taifa la
China(TASAFIC) uliofanyika mjini Wuhan, jimbo la Hubei hivi karibuni.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano Mkuu wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki
Na Happiness Shayo- China.
Balozi
wa Tanzania nchini China Mhe Mbelwa Kairuki amewataka Watanzania
wanaosoma katika Taifa hilo kutumia fursa hiyo kuunga mkono juhudi za
Tanzania kuelekea Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza
katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma
katika Taifa la China(TASAFIC) uliofanyika hivi karibuni katika mji wa
Wuhan, Jimbo la Hubei.
Balozi
Kairuki alisema kuwa yapo maeneo kadhaa ambayo Watanzania hao wanaweza
kutoa michango yao katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya
Tano kwenye ujenzi wa Viwanda ili sekta hiyo isaidie na kuleta tija
katika ukuaji wa Uchumi.
Akizungumzia
kuhusu sekta ya Utalii, Balozi Kairuki aliitaja China kama soko jipya
wanalopatikana watalii na kwamba kwa mwaka 2016 ni Wachina Millioni 120
waliokwenda nje ya nchi kutalii sawa na idadi ya watu wote wa nchi za
Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi na Rwanda, idadi inayoonekana ni kubwa
sana,ambapo kwa mwaka huo huo ni watalii 30,000 walipokelewa Tanzania
kutoka China.
“Zipo
hatua kadhaa ambazo sasa zimechukuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
China, hivi sasa tunazungumza na kampuni kubwa inayomiliki mitandao ya
kijamii hapa ya China ya TENCENT ili tuweze kutumia mtandao wao wa QQ
kurusha vivutio vyetu vya utalii hapa China mubashara, lakini pia mwezi
huu tulikuwa na Mazungumzo na Serikali ya China kuwajulisha nia ya
shirika letu la ndege la Air Tanzania kuanza safari za moja kwa moja
kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou.
Matarajio yetu ni kuona kwamba ifikapo Mwezi Septemba mwakani lengo hilo linatimia. Vilevile tumeanza kuzungumza na Mamlaka za China kuangalia uwezekano wa mashirika ya ndege ya China kuifanya Tanzania kuwa kitovu (HUB) ya safari zao Barani Afrika. Maana yake nini? Ndege kadhaa za China zinazokwenda Afrika zitakuwa zitasimamna (stopover) pale Dar es salaam au KIA au Mbeya (Songwe) kwa ajili ya kujaza mafuta na kupata huduma nyinginezo. Alisema Balozi Kairuki.
Matarajio yetu ni kuona kwamba ifikapo Mwezi Septemba mwakani lengo hilo linatimia. Vilevile tumeanza kuzungumza na Mamlaka za China kuangalia uwezekano wa mashirika ya ndege ya China kuifanya Tanzania kuwa kitovu (HUB) ya safari zao Barani Afrika. Maana yake nini? Ndege kadhaa za China zinazokwenda Afrika zitakuwa zitasimamna (stopover) pale Dar es salaam au KIA au Mbeya (Songwe) kwa ajili ya kujaza mafuta na kupata huduma nyinginezo. Alisema Balozi Kairuki.
Kwa
upande wa Sekta ya Elimu Balozi Kairuki amewataka Watanzania wanaosoma
katika taifa hili kuendelea kutafuta fursa za masomo hapa China kwa
faida ya watanzania wengine na kwamba China ina vyuo takribani 2000
hivyo jambo hili sio jukumu la Ubalozi pekee, hususani maeneo yenye
upungufu katika taifa letu, huku akitoa kipaumbele kwenye kozi za
Kilimo na Uhandisi ambazo alizitaja kama nguzo muhimu katika Uchumi wa
viwanda.
“Kilimo
ni uti wa mgongo wa taifa letu. Kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 70
ya Watanzania wote ambao wengi wao wapo vijijiji. tunahitaji kilimo
kuzalisha malighafi za viwandani na hatuwezi kutimiza malengo ya kujenga
uchumi wa viwanda bila kufanya maboresho makubwa ya sekta ya
kilimo.Lakini pia tunaamini kabisa Mtanzania anayekuja kusoma uhandisi
hapa China mbali na elimu ya darasani, atapata pia exposure kubwa ya
kazi za uhandisi zinazofanyika hapa China na tayari tumeanza kuzungumza
na makampuni ya ujenzi ya hapa China kuyaomba yatoe fursa kwa wanafunzi
watanzania kufanya elective programs ili mshiriki kwenye miradi mikubwa
ya ujenzi.
Aidha
, Balozi Kairuki aliwataka Watanzania hao kutumia fursahizo kuvutia
wawekezaji . “Tunahitaji uwekezaji wa mitaji, teknolojia na ujuzi katika
kuanzisha na kuendesha viwanda nchini na kazi yetu kubwa ni kuendelea
kuvutia uwekezaji wa viwanda kutoka China sambamba na kutafuta
teknolojia rahisi na nafuu zinazoweza kupelekwa nyumbani kuwezesha
watanzania kufanya shughuli za uzalishaji.
Hivi sasa uwekezaji nchini kutoka China unakadiriwa kufikia dola za kimarekani Bilioni 3.7. Lengo letu ni kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 5 ifikapo mwaka 2020. Wanafunzi wanaosoma China ni muhimu kuwatumia pia Wahadhiri katika vyuo vyao, ambao wengi wao wanayo mahusiano na wa kichina ambao wana mitaji na wangependa kuwekeza barani Afrika. Alisema Kairuki.
Hivi sasa uwekezaji nchini kutoka China unakadiriwa kufikia dola za kimarekani Bilioni 3.7. Lengo letu ni kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 5 ifikapo mwaka 2020. Wanafunzi wanaosoma China ni muhimu kuwatumia pia Wahadhiri katika vyuo vyao, ambao wengi wao wanayo mahusiano na wa kichina ambao wana mitaji na wangependa kuwekeza barani Afrika. Alisema Kairuki.
Akihitimisha
hotuba yake Balozi kairuki aliwataka Watanzania hao kuheshimu
tamaduni na sheria za taifa la China,Kila mmoja kutambua kusudi la uwepo
wake hapa nchini kuepuka maisha ya kifahari, Kuchukua tahadhari juu ya
Madawa ya Kulevya, kuepuka migomo kwa kuzingatia taratibu na sheria za
vyuo vyao,kutunza na kulinda Afya zao na kwa wanafunzi wa shahada za
uzamili na Uzamivu aliwataka kufanya Tafiti zenye tija kwa Taifa la
Tanzania.Ingawa pia alitumia nafasi hiyo kuwatambua Watanzania kadhaa
wanaosoma katika Taifa hilo kutambua michango wao mkubwa walioutoa kwa
manufaa ya Tanzania kupitia sekta ya Kilimo na Uhandisi.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Bw. Remidius Emmanuel
alisema Mkutano huo ulilenga kuwakutanisha Watanzania wote wanaosoma
katika taifa la China kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali juu ya
Elimu na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo lakini pia kutengeneza
sauti ya pamoja na kuona namna bora zaidi ya kutumia fursa hiyo ya uwepo
wao katika taifa hilo kwa manufaa ya Tanzania.
“Tunamshukuru
sana Balozi wetu Mhe. Mbelwa Kairuki wakati wote amekuwa karibu na sisi
lakini kutumia muda mwingi kuzifanya taaluma zetu katika matumizi
mapana yanayolenga kuendana na sera za nchi yetu hususani kipindi hiki
ambacho taifa letu liko kwenye kasi ya kuelekea uchumi wa kati.Kwa hiyo
Madaktari,Wataalam kilimo ,Wahandisi,Wachumi na wataalam wengine wote
sasa wanaelekeza taaluma zao kwa manufaa ya taifa letu” Alisema
Remidius.
Mapema
akisoma Taarifa ya Mkutano huo Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw,Hussein
Mtoro alisema mbali na kuwaunganisha Watanzania kwa Umoja wao ,
Shirikisho hilo linalo jukumu la kuhakikisha Watanzania wote wanaosoma
katika taifa la China wanatoa mawazo,fikra zao ,kwa kutumia taaluma na
uzoefu wao kwa manufaa ya Taifa la Tanzania.
"Shirikisho
limeweza kuweka mazingira mazuri kwa Watanzania wanaowasili China kwa
mara ya kwanza kila mwaka, tunaendelea kutatua changamoto kwa baadhi ya
mawakala wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwatelekeza na kuwalaghai
wanafunzi wapowaleta katika taifa hili, lakini tunajivunia kuwa na
wataalamu mbalimbali ambao kutoa michango wa moja kwa moja kwa taifa
letu, Mfano wataalam kutoka fani za Kilimo na uhandisi".Alisema Bw.
Hussein
Mkutano
huo Ulihudhuriwa na Watanzania wanaosoma katika Taifa la China na
baadhi ya watumishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China.
No comments:
Post a Comment