Na Mwandishi wetu,
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria na kujizatiti
kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye
tija katika Sekta ya Kilimo kwa wakulima wa kanda ya ziwa na Tanzania
kwa ujumla ili kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Dhamira
hiyo imewekwa wazi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo,
Bibi Rosebud Kurwijila wakati akitembelea miradi mbalimbali ya kilimo
mkoani Mwanza hivi karibuni.
Bibi
Kurwijila alisema kuwa katika kutekeleza mkakati wa kuwafikia wakulima
wengi zaidi nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
imejipanga kutoa huduma kupitia kongane mpya nane (8) ili kuongeza tija
kwa wakulima nchini.
“Kongane
ni njia ya kimkakati ya kijiografia yenye kujikita katika shughuli za
kilimo zinazohusiana, wasambazaji, na taasisi zinazohusishwa katika
kujenga usawa wa moja kwa moja miongoni mwa wadau, hivyo ili kukidhi
mahitaji ya wakulima nchini, benki ya kilimo itawafikia kupitia njia
hii,” alisema.
Aliongeza
kuwa kongane ya Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Mwanza,
Kagera, Mara, Shinyanga, Geita na Simiyu itatoa fursa ya ushindani kwa
njia endelevu ili kuchagiza uhusiano na ushirikiano katika uongezaji wa
thamani hasa katika makundi mbalimbali ya minyororo ya thamani, pamoja
na taasisi na mamlaka za udhibiti zinazosaidia sekta ya kilimo nchini.
“Tunaamini
kuwa kupitia mifumo thabiti ya kongane kwenye ongezeko la thamani Benki
itawajengea uwezo wakulima katika kuboresha ujuzi katika mapatano na
kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma pia kuwapatia wakulima katika
vikundi faida za kiuchumi kwa kuzingatia nguvu ya masoko ya mazao yao,”
aliongeza.
Kwa
mujibu wa mpango kazi wa Benki hiyo, dhana ya Kongane imeandaliwa kwa
kutokana na mgawanyo wa kiokolojia kwenye kilimo kuzingatia kanda
zilibainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II
2016/17-2020/21) ambapo mikoa imegawanywa ili kurahisisha utoaji wa
huduma na mapendekezo ya teknolojia kwenye mifumo sawa ya uzalishaji.
Kongane hizi zimezingatia utendaji wa kila mnyororo wa thamani ya kilimo
na faida za linganifu katika kila mkoa katika uzalishaji.
Mpango
kazi huo unaweka bayana kuwa matumizi ya Kongane yanalenga kuchagiza
ufanisi katika kuimarisha minyororo ya thamani hasa wakati hakuna
misingi thabiti katika kuendeleza minyororo hiyo ambayo inajumuisha
kuanzia uzalishaji, usindikaji, usafiri, usambazaji, kuwezesha mazingira
na soko. Hivyo uhitaji wa kuingilia kati juhudi hizi kutoka kwa wadau
wengi ambao hawawezi kutatua suala lolote kwa pekee.
Akizungumzia
mgawanyo wa mazao yatakayopata kipaumbele kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa,
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu
Chacha alisema kuwa uteuzi wa minyororo ya thamani ya kipaumbele katika
kila eneo umechukulia mchango wa mnyororo wa thamani katika usalama wa
chakula, athari chanya kwa wakulima wadogo wadogo, mchango katika
mikakati ya maendeleo ya kitaifa (hasa uendelezaji wa viwanda) - mpango
wa maendeleo ya miaka mitano, soko la ndani na mauzo ya nje.
“Kwa
mikoa ya Kanda ya Ziwa mazao ya kipaumbele ni Mihogo, Mpunga, Mikunde,
Ng’ombe wa Nyama na Maziwa, Pamba, Miwa na Samaki,” alisema.
Bw.
Chacha aliongeza kuwa Benki ya Kilimo inaamini kuwa kupitia Kongane
wakulima wa watafikiwa kwa haraka kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi
kubwa na yenye maeneo tofauti ya kimazingira/kilimo (Makundi) ambayo
yana faida linganifu kwa ajili ya kuzalisha mazao maalum au seti ya
bidhaa (mazao, mifugo, uvuvi).
TADB
iliyozinduliwa rasmi mnamo tarehe 08 Agosti 2015 imeanzishwa kwa
madhumuni makubwa mawili ya kusaidia utoshelezi na usalama wa chakula
endelevu nchini Tanzania; na kuchagiza mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo
cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa
uchumi na kupunguza umaskini.
Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kulia) akitoa
maelezo juu ya uchakataji wa nyama kwenye Kiwanda hicho kwa ugeni kutoka
Benki ya Kilimo. Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia).
Ugeni
huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi
Rosebud Kurwijila (wapili kushoto) wakiangalia namna ng’ombe
anavyoandaliwa mara baada ya kuchinjwa.
Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (wapili kushoto)
akionesha soseji zilizokuwa katika hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni
wageni kutoka Benki ya Kilimo.
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB wakiangalia bidhaa mbalimbali
zinazosindikwa na Kiwanda cha Chobo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila na wajumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi Bw. Joseph Mutashubilwa (wapili kulia) na Bw. Dome
Malosha (kulia).
Mmiliki
wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo (mbele) akiwaonesha
mahala maji taka yanapochujwa ili kulinda mazingira ya kiwanda.
Wanaongalia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi
Rosebud Kurwijila (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki
hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto). Wapili kushoto ni Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia)
akiangalia pembe ya ng’ombe kutoka Kiwanda cha Chobo. Kwa mujibu wa
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kushoto)
pembe hizo uuzwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment