Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(Katikati) akiwa amewasili katika Viwanja vya Kili Golf Jumapili Mkoani
Arusha kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf
Kulia ni Katibu Wake Bw. Andrew Magombana na kushoto ni Bw. Chris Martin
Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Bw. Bastiaan
Bruins (Kushoto) baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya
kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katikati ni Makamu wa
Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union) Bw. Chris Martin.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (
wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa
mashindano ya Wazi ya Kili Golf Mkoani Arusha.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akitoa risala kwa washiriki wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf
katika halfa ya kufunga mashindano hayo jana Mkoani Arusha.
Mshiriki
kutoka Kenya Bw. Edwin Mudanyi akijiandaa kupiga mpira wakati wa
fainali wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha
ambapo jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi,
Zambia, Afrika ya Kusini na Tanzania walishiriki.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akimpa mkono wa hongera mmoja wa washindi wa kwanza Bw. Victor Joseph
kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa mashindano ya Wazi ya Tanzania
Kili Golf jana Mkoani Arusha.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).
Serikali
imeahidi kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa mchezo wa Golf nchini
katika kuhakikisha mchezo huo unafundishwa kuanzia ngazi ya chini ili
kuandaa wachezaji bora wa kimataifa wataoiwakilisha nchi katika
mashindano hayo duniani.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe alipokuwa akifunga mashindano ya Kili Golf Mkoani
Arusha ambapo ameeleza kuwa mchezo huo ni wa muhimu ukazingatiwa katika
kukuza sekta ya michezo.
“Mchezo
huu wa Golf ni mzuri sana kwa kuwa unakusanya watu wa tamaduni
mbalimbali na kuwaleta pamoja nami naahidi kuwa Wizara yangu
itahakikisha inashirikiana kwa karibu na wadau wa Golf nchini ili
kuukuza zaidi” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.
Mhe.
Dkt. Mwakyembe ameongoza kwa kuwataka washiriki wa mchezo huo kuwa
mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi na
kuhamasisha vijana wengine kuwa na moyo wa kujifunza.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Arusha Bw.Bastiaan Bruins amesema kuwa
lengo la mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unafahamika kwa watu
wengi na kuondoa dhana iliyojengeka kuwa ni mchezo wa kitajiri.
“Mashindano
haya ni kuwapa hamasa watanzania kuupenda,kujifunza na kuelewa mchezo
huu wa Golf ambao ni mchezo rahisi sana na unachangamasha akili huku
ukiwaleta watu kutoka sehemu mbalimbali kuwa kitu kimoja” amesema
Bw.Bruins.
Kwa
upande wa washiriki wa mashindano hayo hususani kutoka nje ya Tanzania
wamewashukuru waandaaji na watanzania kwa ukarimu, upendo,ushirikiano
na umoja waliouonyesha huku wakiahidi kushiriki tena mashindano mwakani.
Mashindano
ya Wazi ya Kili Golf Tanzania yalifunguliwa rasmi Novemba 10 mwaka huu
yakiwa na jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Malawi,Zambia, Afrika ya
Kusini, Uganda , Kenya na wenyeji wao Tanzania huku nafasi ya kwanza
ikichukuliwa na washindi wawili baada ya kutoka sare katika mchezo wa
mwisho ambao ni Bw. Edwin Mudanyi kutoka Kenya na Bw. Victor Joseph
kutoka Tanzania.
No comments:
Post a Comment