
Kauli hiyo
waliitoa wakati wakichangia semina ya wabunge juu ya jukumu la Bunge
katika kufuatilia kikamilifu matumizi ya Serikali yaliyofanyika kwa
kamati saba za Bunge.
Kamati hizo ni
Kamati ya Bajeti, Kilimo, Mifugo na Maji, Viwanda, Biashara na
Mazingira, Huduma za Jamii, Utawala na Serikali za Mitaa na Hesabu za
Serikali za Mitaa.
Akizungumza
katika semina hiyo, Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alisema
wabunge wamekuwa waoga kusemea tofauti na Bunge la 10 na kwamba hoja
zinajengwa kisiasa na wengine wanapohoji wanaambiwa hawatapelekewa fedha
majimboni.
Alisema jambo
linalowafanya wabunge kutosema yale wanayoyataka wananchi ni siasa
kuingia bungeni tofauti na mabunge yaliyotangulia ambapo wabunge
walikuwa wakiacha siasa lango kuu la kuingilia bungeni.
“Jambo hili
linaweza kuwa linasababishwa na viongozi wa bunge ama serikali ambapo
hoja zenye manufaa zinaweza kupelekwa bungeni, lakini wakaamua
kuziua,”alisema Selasini.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Hassan Turky, alisema mambo yote
waliyoelezwa wanayajua, lakini kuna kitu kinachomoza bungeni na
kinaondoa uhai wa bunge.
“Hasa unapohoji
na kudadisi basi na wewe unaitwa na kuhojiwa na kudadisiwa," alisema
Turky, "kwa hiyo wabunge wote wanakuwa waoga wa kuuliza maswali".
"Sasa sijui kama utaratibu huu utafanya haki itendeke?”
Aliomba viongozi wa Bunge wakaliangalie hilo na kwamba endapo wakisimamia serikali vizuri wataweza kutekeleza majukumu yao.
Naye Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara alisema kuwa tatizo lililopo ni Bunge kutofanya kazi inavyotakiwa.
“Inafikia Bunge
mtu akisema hapana, waliosema hapana wasipewe fedha za maendeleo kwenye
majimbo yao wakati hayo mambo hayakuwapo,” alisema Mbunge huyo.
Alisema wabunge sasa wanaogopa kuisema au kuikosoa serikali licha ya kuwa Bunge limeundwa ili kusema kero za wananchi.
“Bunge limebaki
kuwa la muhuri na sio Bunge, na sisi hapa tunakuja kwa ajili ya posho
na mishahara tu tuliyoambiwa,” alisema Mbunge huyo.
Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) alisema nguvu ya Bunge ya kuisimamia serikali ni ndogo kutokana na ukosefu wa fedha.
“Ili tuweze
kuwa na mchango madhubuti lazima tujengewe uwezo wa kushughulikia
taarifa mbalimbali, Bunge lihakikishe linatujengea uwezo kwenye nyanja
mbalimbali wabunge ili kuisimamia serikali ipasavyo kwenye masuala
mbalimbali ikiwamo bajeti,” alisema.
Mbunge wa Ileje
(CCM), Janet Mbene ambaye alikuwa mwenyekiti wa semina hiyo, alisema
kwa umoja wao wabunge wakisimama kwa pamoja serikali itawasikiliza na
hawatafanya kazi kwa woga
No comments:
Post a Comment