Afisa
mwandamizi wa masoko wa Dar es Salaam wa DSE, Mary Kinabo akizungumza
na waandishi wa habari
SOKO
la Hisa Dar es Salaam(DSE) limesema thamani ya mauzo ya hisa imepungua
kutoka bilioni 20 kwa wiki iliyoishia Oktoba 27 hadi bilioni 3 ya
wiki iliyoishia Novemba 3 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa leo na Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa Dar es Salaam wa DSE,
Mary Kinabo wakati anawasilisha yaliyojiri kwenye soko hilo kwa wiki
iliyoishia Novemba 3 mwaka huu.
Amesema
idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa milioni 1.6
ya wiki iliyoishia Oktoba 27 hadi hisa milioni 3.5 ya wiki iliyoishia
tarehe 3 mwezi Novemba, 2017.
"
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya soko la hisa ni TCC (41%),
Tanzania Breweweries Ltd (27%), Benki ya CRDB (16%) na VODA (11%),
amesema.
Amebainisha
kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko
umepungua kwa Sh bilioni 217 kutoka Sh bilioni20.5 wiki iliyopita hadi
Sh Trilioni 20.2 wiki ilioyoishia Novemba 3 mwaka huu na kwamba punguzo
hilo limetokana na kupungua kwa bei za hisa za KA (8%), JHL (8%), CRDB
(6%) na TBL (5%).
Amessisitiza
kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kutoka Sh bilioni
112 kutoka Trilioni 10.163 hadi kufikia Sh trilioni 10.051 wiki hii
ikisababishwa na kupungua kwa bei za hisa za kampuni za CRDB (6%) na TBL
(5%).
Amefafanua
kuwa mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia Novemba 3 yalikuwa Sh
bilioni 15.7 kutoka Sh milioni 500 wiki iliyopita ya Oktoba 27 mwaka
huu.
Ameongeza
kuwa mauzo hayo yametokana na hatifungani 11 za Serikali na za
Makampuni binafsi zenye jumla ya thamani ya Sh bilioni 15.7.
Pia
amesema kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko hilo
yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 23 kutoka pointi 2,124 hadi 2,101
kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Shrika la Ndege la Kenya(KA)
Jubilee Holdings ltd (JHL), CRDB na TBL.
Katika
hatua nyingine, amesema kiashiria cha kampuni za ndani (TSI) kimepungua
kwa pointi 43 kutoka pointi 3,876 hadi 3,833 sababu ya kushuka kwa bei
za hisa za CRDB na TBL..
Wakati
huo huo, ameanisha kuwa kiashiria cha sekta ya viwanda kimepungua kwa
poiti 77 kutoka pointi 5,379 hadi 5,303, kiashiria cha huduma za
kibenki na fedha kimeshuka kwa pointi 33 kutoka pointi 2,497 hadi 2,464
huku cha Sekta ya huduma za kibiashara wiki hii kimebaki kama awali
kwenye wastani wa pointi 2,462.
No comments:
Post a Comment