MBUNGE wa Viti Maalum katika
Manispaa ya Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Anatropia
Theonest alieshika kombe kabla yakuwakabidhi washindi wa mashindano hayo
Mmoja wa viongozi wa mashindano hayo akiongea jambo na washiriki mapoja na mashabiki wa mchezo huo.
MBUNGE wa Viti Maalum katika
Manispaa ya Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Anatropia
Theonest ameahidi kudhamini timu ya vijana ya Argexas ya Buguruni jijini Dar es
Salaam hadi kuiwezesha kufikia Ligi Kuu.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam juzi baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano ya Kombe la Anatropia
Segerea ambayo yeye ndio muandaaji wake, Anatropia alisema amelazimika kuandaa
mashindano hayo ili kuwaweka karibu vijana na kwamba timu ya Argexas iliyoibuka na ubingwa
ataifadhili ili kuiwezesha kufika mbali hadi kucheza ligi kuu.
Alisema sambamba na kuisaidia
pia atakuwa akiibua vijana mbalimbali
wenye vipaji ambao watakuwa wakiongeza nguvu katika timu hiyo ambayo anaamini
itafika mbali kutokana na uwezo mkubwa walioonyesha.
“Natamani hii timu ije iwe timu
bora katika Manispaa ya Ilala na pia nitafurahi zaidi pale nitakapoona inafika
kucheza katika ligi kuu,” alisema Anatropia.
Alisema anatarajia kuyafanya
mashindano hayo kuwa ya muendelezo ili kuweza kutimiza lengo la kuwaweka karibu
vijana ikiwa ni pamoja na lile la kupinga unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya
watoto katika Manispaa ya Ilala ifikapo 2020.
Alisema hadi kufika hatua ya
fainali, mashindano hayo yalishirikisha timu 24 na kwamba mshindi wa kwanza
alizawadiwa ng’ombe, kombe, jezi na mpira mmoja huku mshindi wa pili akipata
mbuzi wawili, jezi na mpira mmoja.
Aliongeza kuwa mshindi wa tatu
alipata jezi na mpira mmoja huku mfungaji bora kutoka katika timu ya Argexas
ambayo ndio bingwa wa mashindano alimzawadia pesa taslimu sh 100,000.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment