Taasisi
ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3
kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la
kuombea fedha kwa ajili ya tafiti. Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi
ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development
Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank
Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam.
Akizungumza
Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives
anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema
kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na
Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya
kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka
mashirika mbalimbali ya kimataifa.
Mkuu
wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa
washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko bora ya
utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Taasisi ya Kimataifa
ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia Taasisi ya Kimataifa ya
Wanazuoni (Think Tank Initiatives-TTI) na kumalizika mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi
watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda
nchini. “Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi
wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo
chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya
maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi Alisisitiza
umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi
hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa
ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda.
Mtalaamu
Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa
ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifungua warsha ya siku
tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu
ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Alisisitiza
kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi
katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa
maeneo ya vijijini. Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu
mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile
gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza
tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti.
Picha
juu na chini ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji Maendeleo
Afrika, Prof. Olu Ajakaiye akielezea namna bora ya utengenezaji wa
maandiko kwa ufupi na kwa usahihi wakati wa warsha ya siku tatu ya
uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kwa washiriki kutoka shirika la
IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER),
REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana iliyomalizika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa
ESRF.
Mtalaamu
Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa
ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia program ya TTI , Julie LaFrance,
amesema kwamba ni muhimu kwa watafiti kuendelea na utafiti endelevu na
wa kina ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii ya watu baada ya
kupata matokeo baada ya utafiti.
Aliongeza
kwamba baada ya semina hiyo watafiti wa ndani watakuwa wamepata uelewa
mkubwa wa kuandika mapendeko thabiti na bora zaidi yenye kuvutia wadau
wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kuanza kuwapa fedha kwa ajili ya
tafiti zenye tija nchini. Warsha hiyo pia iliwakutanisha watafiti kutoka
Taasisi ya IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa
uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na chuo cha Jamii kutoka Ghana.
Mtaalamu
wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akiwasilisha mada umuhimu wa
jinsia kama moja ya kipengele muhimu katika kuandaa maandiko mbalimbali
ya kitafiti katika kushawishi wabia wa maendeleo kutoa ruzuku za
uatfiti.
Mtalaamu
Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa
ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifurahi jambo wakati
mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni
mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3095" align="aligncenter"
width="1404"]
Mkuu
wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akichangia jambo wakati
wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku
iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank
Initiatives-TTI.
Prof.
Peter Okidi-Lating (aliyesimama) kutoka Chuo Kikuu cha Makerere
akipitia meza za vikundi kazi vya washiriki wa warsha ya siku tatu ya
uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa
ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.
Mtaalamu
wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati
wa zoezi la vikundi kazi katika meza ya washirki kutoka ESRF katika
warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu mshiriki Aldegunda Ngowi kutoka ESRF na chini ni mshiriki kutoka
Ghana wakichangia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya
uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kutoka Shirika la IPAR- Senegal,
Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF,
STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana
Mkuu
wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akibadilishana mawazo
na Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance wakati warsha
ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na
ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.
No comments:
Post a Comment