Katibu
tawala wa mkoa wa Mtwara akisisitiza jambo kwa wenye wajumbe wa kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara na baadhi ya wageni waalikwa
kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa
kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara ambalo linatarajiwa kuanza rasmi
mwanzoni mwa wiki ijayo
Kaimu
mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bi. Rose Joseph
akiwasilisha salamu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndg,
Andrew Wilson Massawe kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara pamoja
na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa zoezi la uzinduzi
wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara.
Mkuu
wa Wilaya ya Mtwara mjini akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi zoezi
la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara na
kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, watumishi wa NIDA
pamoja na wageni wengine waalikwa.
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
pichani wakisikiliza jambo kutoka kwa mwakilishi Mkuu wa mkoa wa Mtwara
wakati wa sherehe ya uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya
Taifa kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Mtwara pamoja na
wageni waalikwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho
vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara
Afisa
usajili msaidizi wa NIDA Ndg. Fredy Mahundi akifanya zoezi la usajili
kwa mara ya kwanza kwa mwananchi wa mkoa wa Mtwara mara baada ya zoezi
la uzinduzi wa usajili kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kukamilika.
Bi
Amina Bakari akichukuliwa alama zake za Vidole ambapo alipata nafasi ya
kuwa mwananchi wa kwanza kusajiliwa kwa mkoa wa Mtwara mara baada ya
zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa
Mtwara kukamilika.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara leo amezindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa
Watu kwa wananchi wa mkoa huo tayari kuanza rasmi kwa zoezi la usajili
kwa wananchi ikihusisha kuchukuliwa picha, saini na alama za
Kibaiolojia.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Mtwara umejipanga na uko tayari kwa
zoezi hilo, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa hali na mali kuhakikisha
hakuna mwananchi yeyote mwenye sifa ambaye ataachwa bila kusajiliwa.
Katika
sherehe za uzinduzi rasmi wa zoezi hilo zilizofanyika makao makuu ya
Mkoa huo Mtwara; zilihudhuriwa na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Meya,
Katibu Tawala Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi wa
Halmashauri zote, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama ngazi ya Mkoa, Watumishi katika ngazi mbalimbali na
vyombo vya Habari.
Akizungumza
kwa niaba ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Bi. Rose Joseph ameeleza Mamlaka imejipanga kuanza rasmi
zoezi hilo Jumatatu tarehe 13 Novemba, 2017 na wanakusudia kukamilisha
zoezi hilo kwa mkoa wa Mtwara kufikia Februari 2018 na kuanza kutoa
namba za Utambulisho NIN sambamba na uzalishaji wa Vitambulisho.
Ziadi
ya wananchi mil 1,250,000 wanatazamiwa kusajiliwa mkoani humo. Mikoa
mingine ambayo usajili umeanza ni Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro,
Singida, Arusha, Shinyanga, Geita, Mwanza, Simiyu, Manyara na Songwe.
No comments:
Post a Comment