Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limedai kuwa lina mashaka
kuhusu uhalali wa udaktari wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa Tajiri
aliyeshinda katika mnada wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi
uliofanyika juzi siku ya Alhamisi kwa kuwaameshindwa kuonyesha vielelezo
kuthibitisha elimu yake ya kiwango cha Ph.D
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa
Kanda ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema wanaendelea na
upelelezi dhidi ya mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Dkt. Louis Shika
na kwamba jana hiyo walikwenda kumkagua nyumbani kwake Tabata Mawenzi.
Kamanda
Mambosasa amesema kuwa Shika hana taaluma ya udakatri na kwamba
inasemekana huenda alitumwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kuharibu
mnada huo baada ya kushindwa kutoa fedha ambazo alidai ziko nje ya nchi.
“Tulipokea
taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Stanley
Kevela, kuwa huko Mbweni JKT wakiwa wanafanya mnada wa hadhara wa kuuza
nyumba za mfanyabiashara Lugumi, alijitokeza mtu anayeitwa Shika ambaye
alishinda mnada huo kwa kutaka kununua nyumba zote tatu, kumbe hakuwa na
fedha,” alisema Mambosasa.
Mambosasa
alisema '‘tajiri’ huyo alitaka kununua nyumba moja ya Mbweni kwa Sh.
bilioni 1.2, nyumba ya pili iliyoko pia Mbweni Sh. milioni 900 na nyumba
ya tatu iliyoko Upanga alishinda na kutaka kununua kwa Sh. bilioni 1.2
na Mtuhumiwa huyo alitakiwa kulipa asilimia 25 ya fedha kwa kila nyumba
lakini hakuwa na fedha ndipo walipomkamata na kumfikisha kituo cha
polisi kwa hatua zaidi.
Aidha,
Kamanda Mambosasa alisema taarifa zinaonyesha kuwa inawezekana Mtu huyo
alitumiwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kwa kuwa alivyotakiwa kutoa
fedha alisema ziko nchini Russia na Lugumi hajulikani mahali anapoishi
kwa sasa.
Pia alisema wanaendelea kumhoji juu ya taaluma ya udaktari aliyoitaja ingawa bado alikuwa hajaithibitisha kwa kutoa vielelezo.
“Amesema
ni daktari lakini hajathibitisha kwa hiyo udaktari wake hadi sasa ni wa
madai, hivyo amefanya kazi wapi hajatuambia. Upelelezi unaendelea na
atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria,” alisema.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, November 11, 2017
Tajiri' Dkt. Shika azua utata mwingine
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment