Aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri
wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa
ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya
rushwa.
Kupitia
mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla
amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa
aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.
Balozi
ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa
kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa
karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa
Waziri na rushwa niliyopokea,"
Hata
hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri
Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba
Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao
"Mhe.
Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana.
Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!"
Kigwangalla.
Hivi
karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari wote
wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji
huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa (aliyemsimamisha
kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya karibu na Prof.
Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na
Utalii wa zamani.
Balozi
Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika uongozi wa
serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka (2012
No comments:
Post a Comment