Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) Koshuma Mtengeti,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
SERIKALI
imejipanga kupunguza mimba za utotoni kwa asilimia 27 kwa kipindi cha
miaka mitano kinachoanzia 2017 hadi 2022 lengo likiwa ni kuhakikisha
mototo wa kike anapata haki yake ya elimu.
Hayo
yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maendeleo ma watoto
kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Margareth
Mussai wakati Kongamano la Mtoto wa Kike , liloandaliwa na Jukwaa la
Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo Uswidi (
Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA).
Mussai amesema kwa sasa serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kotokomeza ukatili wa kijinsi kwa upande Mimba za Utoto.
“Katika
Mpango huu tumeanza kupunguza mimba kwa asilimia 27 kwa watoto na
tunaamini mpango huu utasaidia kundokana na tatizo hili”Amesema
Amesema
katika kutekeleza mpango huu, Serikali itashirikiana Taasisi zisizo za
Kiserikali katika kuhakikisha wanapunguza Mimba za Watoto.
Hata
hivyo , Mussai amewataka Watoto wa Kike kujitambua wenyewe kwa
kujiepesha na mambo yasio faa ambayo yatapelekea kuongezeka mimba za
watoto ambapo amedai zimechangiwa na watoto hao kujiingiza kwenye
makundi yasioa faa.
Kw
upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti, amesema
lengo la kongamano hilo ni kuwapatia fursa watoto wa kike kukurana na
Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Uswid ambapo watapata fursa ya
kuelezea mafunzo mbali mbali waliyopata kutokana na utekelezaji wa
miradi mbali mbali ya CDF.
Amesema
miradi hiyo ni pamoja na miradi ya kutokomeza, mimba za utotoni, ndoa
za utotoni, ukatili wa kijinsia na kuonesha kazi za ujasiriamali
walizozifanya ikiwa kama mafanikio ya miradi ya CDF.
“Vile
vile katika kongamano hili, wanaume na wavulana wakiwa kama mabalozi wa
CDF watapata fursa ya kuelezea ni kwa namna gani wanafanya kazi za
kuelimisha jamii pamoja na vijana rika juu ya madhara ya ukatili wa
kijinsia, ukeketaji, mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni ili
kufikia dhana ya Taifa ya kuleta usawa wa kiiinsia,” amesema Mtengeti.
Mkurugenzi
Mwandamizi kutoka SIDA Carin Jamtin, amesema shirika lao limekuwa
likitetea haki za woto kwa kuhakikisha watoto wakike na kiume wanakuwa
na haki sawa katika jamii hususani haki ya kupata elimu.
No comments:
Post a Comment