Mechi
namba 16 Kundi A (Friends Rangers 1 v African Lyon 1). Klabu ya African
Lyon imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya
mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya
14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 20 Kundi A (Mgambo JKT 1 v Mshikamano 0). Klabu ya Mgambo
JKT imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki
wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu
Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 21 Kundi A (Kiluvya United 2 0 v Mshikamano 1). Klabu ya
Kiluvya United imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa
kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume
na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Faini hiyo ni kwa mujibu
wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 24 Kundi A (Friends Rangers 0 v JKT Ruvu 3). Klabu ya
Friends Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika tano baada ya
kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1)
ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 28 Kundi A (Mgambo JKT 2 v Ashanti United 1). Klabu ya
Mgambo JKT imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika
uwanjani kwa dakika 13. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya 14(3) ya
Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 15 Kundi B (KMC 1 v Mbeya Kwanza 0). Mchezaji Stephano
Mwasika wa KMC amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000
(laki tatu) kwa kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa Mbeya Kwanza.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la
Kwanza kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 17 Kundi B (JKT Mlale 1 v Polisi Dar 1). Klabu ya JKT
Mlale imepewa Onyo Kali kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya
mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya
14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Klabu ya Polisi Dar imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa
kufika uwanjani kwa dakika 15. Adhabu hiyo ni utekelezaji wa Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 19 Kundi B (Coastal Union 1 v Polisi Tanzania 1).
Wachezaji Athuman Idd Chuji wa Coastal Union na Shabani Stambuli wa
Polisi Tanzania wamesimamishwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh.
300,000 (laki tatu) kila mmoja kwa kosa la kupigana uwanjani. Adhabu
dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza
kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 21 Kundi B (Mbeya Kwanza 0 v JKT Mlale 0). Klabu ya JKT
Mlale imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kutokana na timu yake
kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu,
kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 23 Kundi B (Mawenzi Market 0 v Mufindi United 1). Klabu
ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
washabiki wake kusababisha mchezo kusimama kwa dakika nne baada ya
kumpiga jiwe Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili. Adhabu hiyo imezingatia
Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 13 Kundi C (JKT Oljoro 1 v Toto Africans 0). Klabu ya
Toto Africans imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao
cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni
kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa
mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 17 Kundi C (Dodoma FC 1 v JKT Oljoro 0). Mwamuzi Said
Pambalelo amepewa Onyo Kali kwa kutochukua hatua dhidi ya wachezaji wa
JKT Oljoro waliokuwa wakifanya vitendo ambavyo ni kinyume na kanuni za
mpira wa miguu. Adhabu dhidi yake ni kwa mjuibu wa Kanuni ya 38(5) ya
Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Mechi namba 26 Kundi C (Transit Camp 1 v Biashara United Mara 0).
Klabu za Transit Camp na Biashara United Mara kila moja imepigwa faini
ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu zao kuonesha vitendo
vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati zikiingiz
uwanjani. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu
kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Klabu ya Transit Camp pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano)
kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho
ya mchezo kupulizwa kwa lengo la kutaka kumpiga Mwamuzi. Adhabu hiyo
imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa
Klabu.
Mechi namba 27 Kundi C (Pamba SC 1 v Rhino Rangers 0). Klabu ya Pamba
imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi
ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni
ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni
ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Nayo klabu ya Rhino Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na washabiki
wa timu yake kutoa lugha za matusi wakati mchezo huo ukiendelea.Mechi
namba 1 Kundi B (Pepsi 1 v Madini 1). Pepsi imepigwa faini ya sh.
100,000 (laki moja) kwa kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi (pre match
meeting), na pia kufika uwanjani. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 9 Kundi B (Madini 1 v Kilimanjaro Heroes 1). Kilimanjaro
Heroes imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kikao cha maandalizi (pre match
meeting) kwa dakika 16. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya
Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 11 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 1 v African Sports 1).
African Sports imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kufika uwanjani, kitendo
ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu
Taratibu za Mchezo. Kanuni hiyo inatika timu kufika uwanjani dakika 60
kabla ya mechi kuanza.
Mechi namba 4 Kundi C (Green Warriors 1 v Mkamba Rangers 0). Klabu ya
Mkamba Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kutohudhuria
kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya
14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 5 Kundi D (Milambo 1 v Area C 0). Milambo imepewa Onyo
Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya
mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la
Pili.
Mechi namba 12 Kundi D (Milambo 0 v Mashujaa 1). Milambo imepewa Onyo
Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya
mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la
Pili.
Pia Mwamuzi wa Akiba, Rajab Said amepewa Onyo Kali kwa kuchelewa
kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi kwa dakika 6. Adhabu ya
Mwamuzi ni kwa mujibu wa Kanuni ya 83(5) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu
Udhibiti wa Waamuzi.
Mechi namba 15 Kundi D (Area C 1 v Mashujaa 0). Mashujaa imepewa Onyo
Kali kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa
mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili. Vilevile timu ya
Mashujaa imepigwa faini ya sh 200,000 (laki mbili) kwa kupitia mlango
usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa
Kanuni ya 14(140 ya Ligi Daraja la Pili.
No comments:
Post a Comment