Meja wa Jeshi la China Xing song akizungumza na waandishi wa habari
Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja wa wadau wa sekta ya afya kutoka China na Tanzania
Waandishi wa habari wakiwa kazini katika hafla hiyo
Madaktari bingwa na wataalamu wa
afya 381 kutoka Jeshi la China wanatarajiwa kuwasili kwa meli katika bandari ya
Dar es salaam tarehe 19 Novemba 2017 kwa ajili ya kufanya matibabu bure kwa
wakazi wa Jiji la DSM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa DSM
PAUL MAKONDA katika kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA
amesema madaktari hao watahudumia wananchi 600 kwa siku ndani ya meli hiyo
ambapo matibabu ya kawaida pamoja na upasuaji utafanyika bure ndani ya meli hiyo na kuwataka
wakazi wa DSM na wananchi wote kwa ujumla kutumia vyema fursa hiyo itakayodumu kwa siku 7. Jijini
hapa pia amesema watanzania wataendelea
kupata neema kama wataendeeleea
kumchagua na kumuamini Rais wetu John Pombe Magufuli katika utawala wake.
FULL VIDIO HAPA
No comments:
Post a Comment