Mkuu wa Mkoa wa Dar es S alaam Paul Makonda wa pili (kushoto) kishikana mikono na Katibu chama cha Mabaharia taifa Kampeni Josiah Mwakibuja baada yakukabidhiwa mfano wa meli katika mkutano wa
mabaharia uliozindulia jana na mkuu huyo wa mkoa hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameahidi kutatua changamoto
zinazowakabili mabahari kwa lengo la kuwawezesha mabaharia kupata kazi
ndani na nje ya nchi.
Makonda ameyasema hayo leo katika
ufunguzi wa mkutano wa mabaharia na kusema changamoto hizi zikitatuliwa
zitaweza kutatengeneza fursa ya watu kupata kazi, kuheshimika na usalama wa
mwajiriwa, uhakika wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi.
"Naamini changamoto zote hizi
ambazo nimeziona zipo kwenye makundi matatu ninaweza kuzitatua na tutaendelea
kushirikiana na kuweka mikakati itayowawezesha mabaharia kunufaika, na
niwahakikishie kwamba tutafanikiwa." Amesema
Aidha amebainisha kuwa zikitokea
nafasi za kazi kwa mabaharia watapewa kipaumbele ili waweze kulinda vyema
rasilimali za nchi na kuepusha kusafirisha Mali za magendo na kusaidia kukuza
uchumi wa taifa kwa kuweza kulipa kodi kikamilifu.
Pia amezungumzia suala la.upimaji
afya bure litakaloanza November 19, mwaka huu litakalofanywa na madktari kutoka
China na watafanya huduma hiyo bure kwa Siku saba na kuwaambia mabaharia ni
fursa kwao kuweza kupima afya kwa lengo la kuchukua taadhari mapema kabla ya
tatizo kuwa kubwa.
"Nawataka wanachi wote wa Dar
es Salaam kujitokeza kwa wingi kupima afya bure November 19 itakayotolewa na
madktari 381,kutoka nchi ya china na ni fursa kwa ninyi mabaharia kupima
afya zenu sitopenda kuona au kusikia Baharia au mkazi wa mkoa huu anaumwa
ghafla tahadhari ni bora kuliko tuba". Amesema Makonda.
No comments:
Post a Comment