Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na
waandishi wa habari leo ofisini kwake alipokuwa akifanya mkutano na Maofisa
kutoka Shirika la umeme TANESCO
Meneja Mwandamizi wa
Tanesco Dar es Salaam na Pwani Eng. Mahende Kugaya akizungumza katika kikao
hicho.
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Picha ya pamoja....... (Picha na Brian Peter)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amefanya kikao na Mameneja wa TANESCO Kanda zote za
Dar es Salaam kujadili mkakati wa kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme na
maboresho ya miundombinu ya Umeme.
Lengo la kikao hicho ni kujadili
mahitaji ya Umeme kwa Mkoa, Kero ya kukatika umeme mara kwa mara (Mgao), Mpango
Mkakati wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na Mvua zinazoendelea kunyesha na
Mpango mkakati wa kuhakikisha Taasisi zote za Umma ikiwemo Shule, Vituo vya
Polisi na Vituo vya Afya vinakuwa na Umeme wa Uhakika.
RC MAKONDA amesema kuwa kukatika kwa
umeme imekuwa kero kubwa kwa wananchi na wakati mwingine kusababisha hasara
hivyo anaamini TANESCO ya sasa chini ya Serikali ya awamu ya Tano itamaliza
kero hizo.
Katika kikao hicho TANESCO
wamemuahidi RC MAKONDA kuwa Umeme utaongezeka kuanzia leo Maeneo yote
yaliyokuwa yakisumbuliwa na upatikanaji wa Umeme hali itakuwa Shwari kuanzia
leo.
Kuhusu suala la Umeme mashuleni
wamekubaliana kuandaa mchanganuo wa mahitaji yanayohitajika kisha kufikisha
ofisini kwake ili kila shule iunganishwe na huduma ya umeme.
RC MAKONDA amewataka kuwa na lugha
nzuri kwa wateja na kufika kwa wakati* pindi wanapopewa taarifa za hitilafu ya
umeme.
Kwa upande wake Meneja mwandamizi
TANESCO Dar es Salaam na Pwani Eng.MAHENDE KUGAYA amemuahidi RC MAKONDA kuwa
watatekeleza yale yote waliyoagizwa kuanzia siku ya leo ikiwemo kutatua kero za
Wananchi za mgao wa Umeme na kufikisha huduma ya umeme kwenye Taasisi zote za
umma ikiwemo Vituo vya Polis, Vituo vya Afya na Shule.
Aidha amemuhakikishia RC MAKONDA
kuwa eneo la Mbagala na Kigamboni kuanzia mwezi Disemba watapata umeme wa
uhakika.
No comments:
Post a Comment